March 29, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Sekondari Pasiansi yaibuka kidedea mpira wa kikapu Mwanza

Na Judith Ferdinand, TimesMajira Online, Mwanza

MASHINDANO ya mchezo wa mpira wa kikaku kwa shule za sekondari Mkoa wa Mwanza yamemalizika huku timu ya shule ya Sekondari Pasiansi ikibuka kinara wa mashindano hayo.

Shule ya sekondari Pasiansi iliibuka mshindi wa mashindano hayo katika mchezo wa fainali baada ya kufunga magoli 73-36 dhidi ya shule ya sekondari Pamba.

Washiriki kwenye mashindano ya mpira wa kikaku kwa shule za sekondari Mkoa wa Mwanza

Akizungumzia na waandishi wa habari mratibu wa mashindano hayo Bahati Kizito,ambayo yalifanyika katika uwanja wa Sabasaba wilayani Ilemela,amesema lengo ni kuibua vipaji vipya vya wachezaji ambao ni wanafunzi shuleni.

Kizito amesema,jumla ya timu nane zimeshiriki katika mashindano hayo ambayo yamekuwa chachu kwa vijana wengi kujitokeza na mwakani wataongeza idadi ya timu zitakazoshiriki huku watachagua wachezaji 30 ambao watashindana katika mchezo wa ‘allstar game’ ambao miongoni mwao watachaguliwa wachezaji 20 kuunda timu ya Mwanza itakayoenda kushindana na mikoa mingine.

“Mashindano hayo tunayoitimisha hapa yalianza Februari 22,mwaka huu, na walitarajia yaishe mwishoni Machi lakini kutokana na ugonjwa wa Corona ,tulihairisha na tulikuwa tumeisha fikia hatua ya nusu fainali.

“Jana mechi za nusu zilichezwa na timu ya Mwanza Sekondari ilicheza na Pamba huku Kiloleli ikicheza na Pasiansi ambapo timu ya Pamba na Pasiansi zilifanikiwa kuingia fainali ambapo Pasiansi imeibuka mshindi katika mashindano haya ambaye amejinyakulia kombe,” amesema Kizito.

Kwa upande wao wachezaji wa timu mbalimbali zilizoshiriki mashindano hayo akiwemo Sydney Mazula,Isaack Michael, walisema changamoto walizonazo ni ukosefu wa vifaa na wachezaji,hivyo wadau na Serikali iwasaidie kutatua changamoto hizo ili kukuza na kuendeleza vipaji vya mchezo huo.

Pia wamewataka wengine wajiunge na kushiriki michezo kwani inafaida nyingi ikiwemo kujenga afya,kuchangamsha mwili na kuepusha vijana kujiingiza kwenye makundi mabaya na ni ajira pia.

Mratibu wa mashindano hayo,Bahati Kizito (mwenye tisheti ya kijivu) akizungumza na baadhi ya wadau kwenye mashindano hayo. Picha zote na Judith Ferdinand