May 10, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Ripoti bajeti ya lishe yazinduliwa

Spika wa Bunge, Job Ndugai akisisitiza jambo kwa Wabunge Vinara wa Lishe, Usalama wa chakula na haki za Watoto Bungeni alipozungumza nao katika mkutano kuhusu masuala ya lishe uliofanyika katika ukumbi wa Msekwa, Bungeni, Jijini Dodoma mkutano ambao ulizindua ripoti ya uchambuzi wa bajeti za lishe kwa nchi za Mashariki na Kusini mwa Afrika. (Picha zote na Ofisi ya Bunge).
Spika wa Bunge, Job Ndugai akizindua ripoti ya uchambuzi wa bajeti za lishe kwa nchi za Mashariki na Kusini mwa Afrika katika ukumbi wa Msekwa, Bungeni, Jijini Dodoma. Kushoto kwake ni Mwenyekiti wa Wabunge Vinara wa Lishe, salama wa chakula na haki za Watoto Bungeni Mhe. Dustan Kitandura, Mtaalam mwandamizi wa lishe kutoka Mradi wa ASPIRES, Tumaini Charles na kulia kwake ni Mkurungenzi Mtendaji PANITA, Tumaini Mikindo. 
Spika wa Bunge, Job Ndugai akionyesha ripoti ya uchambuzi wa bajeti za lishe kwa nchi za Mashariki na Kusini mwa Afrika aliyoizindua katika ukumbi wa Msekwa, Bungeni, Jijini Dodoma. Kushoto kwake ni Mwenyekiti wa Wabunge Vinara wa lishe, usalama wa chakula na haki za Watoto Bungeni,Dustan Kitandura, Mtaalam mwandamizi wa lishe kutoka Mradi wa ASPIRES, Tumaini Charles na kulia kwake ni Mkurungenzi Mtendaji PANITA, Tumaini Mikindo. 
Kikundi cha Wabunge Vinara wa Lishe, Usalama wa Chakula na Haki za Watoto Bungeni wakimsikiliza Spika wa Bunge Mhe Job Ndugai alipozungumza nao katika mkutano kuhusu masuala ya lishe uliofanyika katika ukumbi wa Msekwa, Bungeni, Jijini Dodoma mkutano ambao ulizindua ripoti ya uchambuzi wa bajeti za lishe kwa nchi za Mashariki na Kusini mwa Afrika iliyoandaliwa na Mradi wa lishe wa ASPIRES ulio chini ya Shirika la Kimataifa la Maendeleo la Marekani (USAID).   
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama, akizungumza na Wabunge Vinara wa Lishe, Usalama wa Chakula na Haki za Watoto Bungeni katika mkutano wa masuala ya lishe uliofanyika katika ukumbi wa Msekwa, Bungeni, Jijini Dodoma.