April 29, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

PSSSF yapongezwa kwa kutumia tehama kuwafikia wananchi

Na Mwandishi Wetu, Arusha


Naibu Waziri katika ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Deogratius Ndejembi amezipongeza baadhi ya taasisi za umma, ukiwemo Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) kwa kuweza kuwafikia wananchi kiurahisi kwa kutumia matumizi ya TEHAMA.

Naibu Waziri katika ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mheshimiwa Deogratius Ndejembi (wa nne kutoka kushoto) akipokea kitabu cha Mwongozo kwa Mwanachama kutoka kwa Afisa Uhusiano Mkuu wa PSSSF, Abdul Njaidi (wa pili kushoto), wakati alipotembelea banda la PSSSF katika Maadhimisho ya miaka kumi ya e-GA, jijini Arusha. Wa tano kutoka kushoto ni Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Dkt. Laurean Ndumbaro na kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa e-GA, Mhandisi Benedict Ndomba.


Ndejembi aliyasema hayo jijini hapa katika hotuba yake ya ufunguzi sherehe za kutimiza miaka kumi ya Mamlaka ya Serikali Mtandao (e-GA) na kikao kazi cha tatu cha serikali mtandao, kinachokutanisha wataalam wa TEHAMA kutoka serikalini


“Leo nimejionea kwenye mabanda pale PSSSF wameweza kuweka App ili kuweza kuona michango inavyokwenda Hivyo nielekeze e-GA kuendelea kufanya tafiti ili kuleta bunifu za mifumo ya TEHAMA itakayoliwezesha taifa kufanikiwa kuimarisha sekta za viwanda, biashara na uwekezaji kulipeleka mbele taifa letu kimaendeleo. Na katika hili nitoe pongezi pia kwa taasisi ambazo tayari zimeweza kuwafikia wananchi kiurahisi Zaidi na kuondoa urasimu wa makaratasi…” alisema Mhe. Ndejembi

Mkurugenzi Mkuu wa PSSSF, CPA. Hosea Kashimba akiwa katika picha ya pamoja na Watumishi wa PSSSF kanda ya Kaskazini-Arusha. Kutoka kushoto ni Hadia Hongoa, Meneja wa PSSSF kanda ya kaskazini Vonness Koka na Cleopatra Luze, wakati wa sherehe za miaka kumi ya e-GA.


Ndejembi amezishauri taasisi nyingine za umma kuitumia TEHAMA ili kuwarahisishia wananchi kupata huduma za serikali kwa haraka. PSSSF ina huduma za PSSSF Kiganjani na PSSSF Mtandaon. Huduma hizi ni suluhisho kwa wanachama, wastaafu na waajiri kuweza kupata huduma popote walipo na muda wowote kwa kutumia simu janja au kompyuta bila kuhitaji kufika kwenye ofisi za PSSSF.

Cleopatra Luse, Mtumishi wa Mfuko katika ofisi ya PSSSF Arusha, akitoa maelekezo kwa Mwanachama jinsi ya kujinga na huduma ya PSSSF kiganjani.