May 6, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Pasiasi mabingwa ‘Inter Schools Basketball Tournarment’

Na Judith Ferdinand, TimeMajira Online, Mwanza

TIMU ya mpira wa Kikapu kutoka shule ya Sekondari Pasiansi imeibuka kinara wa mashindano ya mchezo huo maarufu kama ‘Mwanza Inter Schools Basketball Tournarment’ baada ya kuwafunga timu ya shule ya Pamba vikapu 73-36 katika mchezo wa fainali.

Mashindano hayo yalifanyika katika uwanja wa Sabasaba Wilayani Ilemela yakishirikisha timu nane yakilenga kuibua vipaji vipya vya wachezaji ambao ni wanafunzi shuleni.

Akizungumzia na baada ya mashindano hayo, Mratibu wa mashindano hayo Bahati Kizito amesema kuwa, mashindano hayo yamekuwa chachu kwa vijana wengi ambao wamejitokeza.

Amesema, watajipanga kuhakikisha idadi ya timu zitakazoshiriki inaongezeka huku ambapo watachagua wachezaji 30 ambao watashindana katika mchezo wa ‘All Star game’ na miongoni mwao watachaguliwa wachezaji 20 ili kuunda timu ya Mwanza itakayoenda kushindana na Mikoa mingine.

“Mashindano haya tunayoitimisha hapa yalianza Februari 22 mwaka huu nawalitarajia yaishe mwishoni mwa mwezi Machi lakini kutokana na ugonjwa wa homa kali ya mapafu unaosababishwa na kirusi vya Corona tulihairisha yakiwa katika hatua ya nusu fainali na timu ya Mwanza Sekondari ilicheza na Pamba huku Kiloleli ikicheza na Pasiansi ambapo timu ya Pamba na Pasiansi zilifanikiwa kuingia fainali na Pasiansi kufanikiwa kuibuka mshindi na kujinyakulia kombe,” amesema Kizito.

Kwa upande wao wachezaji wa timu mbalimbali zilizoshiriki mashindano hayo akiwemo Sydney Mazula, Isaack Michael, wamesema licha ya kushiriki mashindano hayo lakini changamoto kubwa zinazowakabili ni ukosefu wa vifaa na wadau na Serikali iwasaidie kutatua changamoto hizo ili kukuza na kuendeleza vipaji vya mchezo huo.

Pia wamewataka wanafunzi wengine kujiunga na kushiriki michezo kwani inafaida nyingi ikiwemo kujenga afya,kuchangamsha mwili na kuepusha vijana kujiingiza kwenye makundi mabaya na ni ajira pia.