May 17, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

NMB yatoa mil.68 kusaidia elimu, afya Musoma

Na Mwandishi Wetu,TimesMajira Online, Mara

BENKI ya NMB imetoa msaada wenye thamani ya zaidi ya Sh.milioni 68 kwa ajili ya kusaidia sekta za elimu na afya mkoani Mara msaada ambao utazinufaisha shule 11 za Msingi na Sekondari pamoja na Hospitali ya kumbukumbu ya mwalimu Nyerere maarufu Kwangwa.

Msaada huo umetolewa kwa wilaya za Musoma na Rorya mkoani humu ambapo unahusisha madawati, vifaa vya kuezekea kwa sekta ya elimu pamoja na vitanda maalum kwa sekta ya afya.

Akizungumza kwa nyakati tofauti wakati wa kukabidhi misaada hiyo katika wilaya hizo, Afisa mkuu wa fedha wa benki hiyo Juma Kimori amesema kuwa benki yake itaendelea kushirikiana na serikali katika kuboresha miundombinu ya Elimu na Afya kwa kutoa misaada ya vifaa kutokana na faida iipatayo kila mwaka.

Kimori ameongeza changamoto za sekta za elimu na afya nchini ni jambo la kipaombele kwa benki kutookana na umuhimu wa sekta hizo katika ustawi wa jamii na kwamba ingawa serikali imekuwa ikijitahidi kwa kiwango kikubwa kuboresha sekta hizo lakini bado ipo haja ya jitihada hizo kuungwa mkono.

“Sisi kama wa wadau tunao wajibu wa kuunga mkono juhudi hizi za maendeleo kwa kusaidia jamii kwani jamii hii ndio imeifanya benki ya NMB kuwa hapa ilipo kwani ni benki kubwa kuliko yoyote hapa nchini na na tutaendelea na kuunga mkono jituhada hizi ili kuhakikisha kuwa kunakuwepo na mafanikio ya hali ya juu katika sekta hizi ili ziweze kuwa mfano ndani na nje ya nchi” amesema.

Kimori amesema kuwa kuwa benki hiyo kwa kutambua changamoto zinazozikabili sekta za afya na elimu nchini tayari imekwishatumia zaidi ya Sh 1.88 bilioni kuanzia mwezi Januari mwaka huu hadi sasa kuzisaidia sekta hizo ambapo kwa mikoa ya kanda ya ziwa msaada huo umezinufaisha shule na vituo vya kutolea huduma za afya 129 huku mkoa wa Mara ukiwa umepokea jumla ya madawati 587,mabati 2,580 na vitanda 8 katika kipindi hicho.

Amewataka wananchi kutumia bidhaa mbali mbali za benki hiyo ili waweze kunufaika nazo huku Meneja wa benki hiyo kanda ya ziwa, Baraka Ladislaus akisistiza kuwa benki hiyo itaendelea kutoa misaada ya hali na mali kwa jamii ili kuboresha maisha.

Afisa Mkuu wa Fedha wa NMB Juma Kimori,akimkabidhi Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Prof Philemon Sarungi Peter(aliyevaa tai nyekundu) viti na meza 50, kwenye hafla iliyofanyika shuleni hapo katika kijiji cha Minigo wilayani Rorya mkoani Mara. Benki ya NMB imekabidhi madawati, viti na meza kwa shule msingi na sekondari, na hospitali vyenye thamani jumla ya zaidi ya Shilingi 68 Milioni mkoani Mara ikiwa ni sehemu uwajibikaji wake kwa jamii

Akizungumza bada ya kupokea msaada huo mkuu wa mkoa wa Mara, Ally Hapi ameishukuru kwa msaada huo huku akizitaka mamlaka husika mkoani humo kuhakilisha kuwa zinaboresha taaluma ili kuongeza ufaulu.

Amesema kuwa mkoa wa Mara hauna mpango wa kuwa na makambi kwaajili ya kuwaandaa wanafunzi walio kwenye madarasa ya mitihani kutokana na ukweli kuwa hivi sasa hakuna uhitaji wa makambi hayo kwani serikali imejitahidi kupambana na changamoto za elimu ikiwemo kuajiri walimu wengi siku za hivi karibuni.

Amesema kuwa mkoa wa Mara umejiwekea malengo ili kuhakikisha kuwa taaluma inaboreshwa hasa ikizangatiwa kuwa kumekuwepo na matokeo yasiyoridhisha katika mitihani ya kitaifa kwa matokeo ya darsa la saba, kidato cha pili na cha nne.

Mkurugenzi wa hospitali ya rufaa ya Mkoa wa Mara, Dkt. Joachim Eyembe amesema kuwa msaada huo utasaidia kuboresha huduma zitolewazo hospitalini hapo hasa ikingatiwa kuwa mwezi ujao hospitali hiyo iliyoanza kutoa huduma Novemba mwa mwaka jana inapanua huduma zake kutoka huduma za mama na mtoto za sasa na kuongeza huduma za kibin..