Na Bakari Lulela,TimesMajira Online
KUTOKANA na mwamko wa wanawake kujitokeza kushiriki masuala ya kugombea uongozi katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu, imedhihirika wakipewa nafasi, wataweza kuonesha vipawa vya hali ya juu vitakavyoleta mabadiliko chanya kwenye ukombozi wa taifa.
Hayo yameelezwa jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi wa Chama cha Wanasheria Wanawake (TAWLA), Tike Mwambipile kwenye semina maalumu iliyokuwa ikiwajengea uwezo wanahabari namna ya kuandika ama kuripoti, taarifa zinazowahusu wanawake katika kufikia malengo yao hususan ya uongozi.
“Wanawake wana uwezo mkubwa katika kukabiliana na masuala mbalimbali ya uongozi ndani ya taifa, ambapo wakipatiwa nafasi wataweza kuleta mabadiliko chanya kwenye jamii zetu,” amesema Mwambipile.

More Stories
Jalsa Salana ya 55 kukutanisha washiriki 5,500
Hospitali ya Wilaya Mwera yapatiwa vifaa vya uzazi
RC atoa kifuta jasho waathirika 44 wa moto