May 13, 2026

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Mtaka:Ruhusuni Maafisa Habari kuhudhuria vikao,mafunzo

Na Mwandishi Wetu,WHUSM

.MKUU wa Mkoa wa Njombe, Anthony Mtaka amezipongeza Wizara na Taasisi za Umma ambazo zinapeleka watumishi wake kwenye mafunzo mbalimbali ndani na nje ya nchi.

Amesema hayo wakati akifunga Kikao Kazi cha 21 cha Maafisa Habari, Mawasiliano, Itifaki na Uhusiano Serikalini kilichohitimishwa leo Mei 10, 2026 mkoani Njombe.

Mtaka ameeleza kuwa, mafunzo hayo yanasaidia kuwajengea watumishi uwezo na ujuzi wa taaluma zao husika.

“Kuna viongozi hawapeleki watumishi kwenye mafunzo au vikao vya kada mbalimbali, hao watu wataongezaje ujuzi wa taaluma zao?” Alihoji Mtaka

Vilevile, ametoa rai kwa waandaaji wa vikao kazi hivyo kupongeza ofisi ambazo zinafanya vizuri. Ofisi za Serikali ambazo zinapeleka watumishi wake kwenye mafunzo mbalimbali ya kada husika.