May 20, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

MSD yamshukuru Rais Samia upatikanaji dawa, vifaa tiba

Na Mwandishi Wetu,TimesmajiraOnline,Tabora

BOHARI ya Dawa (MSD) Kanda ya Tabora imemshukuru Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa maboresho makubwa katika sekta ya afya, hususani katika upatikanaji wa dawa na vifaa vya afya.

Akizungumza hivi karubuni mkoani hapa, Kaimu Meneja wa MSD Kanda ya Tabora, Adonizedeck Tefurukwa, amesema kanda hiyo inahudumia mikoa ya Tabora, Kigoma na Katavi ikiwa na jumla ya halmashauri 21 na vituo 701.

Tefurukwa ameeleza kuwa maboresho hayo yameiwezesha MSD, kusambaza dawa na vifaa vya afya mara sita kwa mwaka, kusambaza vifaa vya kupunguza uzazi pingamizi CEmONC ambapo awamu ya kwanza vituo vinne vimefikiwa, ya pili vituo 10 na ya tatu vituo saba, hospitali za wilaya nane, huku fedha ya UVICO-19, ikihudumia hospitali za Mikoa ya Kigoma na Katavi.

Amesema katika kutekeleza majukumu manne ya Bohari hiyo ambayo ni uzalishaji, ununuzi, utunzaji na usambazaji imekuwa ikihakikisha uhusiano na wateja unaimarika.

Amesitiza kuwa katika kuhakikisha uhusiano huo unakuwa bora, wamekuwa wakikutana na wateja mara kwa mara kwa ajili ya kujadili changamoto zilizopo na hospitali kupewa vifaa vya afya hata pale wanapopungukiwa na fedha.

“Katika kipindi cha robo mwaka 2023/2024 MSD Tabora mauzo ya Julai ni asilimia 100, Augosti 126 na Septemba ni 104 hali ambayo inathibitisha kuwa upatikanaji wa dawa na vifaa vya afya ni mzuri,”amesema.