Na Mwandishi Wetu,TimesMajira
WAZIRI Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt. Mwigulu Nchemba amekagua ujenzi wa kituo cha kupokea na kupoza umeme cha Imalilo mkoani Simiyu ambapo ameeleza kukamilika kwa mradi huo kutafungua fursa za uwekezaji na kuboresha huduma ya upatikanaji wa umeme kwa wananchi.
Mwigulu ameyasema hayo Septemba 14, 2026 katika eneo la mradi wa Imalilo wakati akikagua utekelezaji wake.
“Nawapongeza sana Wizara ya Nishati kwa kutekeleza mradi huu kupitia TANESCO kwa kutumia wataalamu wa ndani hongereni sana” amesema Dkt. Mwigulu

Dkt. Mwigulu akizungumzia kuhusu ujenzi wa njia ya kusafirisha umeme kutoka Ibadakuli, Shinyanga hadi Imalilo, Simiyu, Dkt. Mwigulu amesema Serikali itatoa fedha kuhakikisha mradi huo unakamalika na kuwa na tija kwa Taifa.
Awali, akitoa taarifa ya utekelezaji wa mradi Mkurugenzi Mtendaji TANESCO Lazaro Twange amesema mradi umetekelezwa kwa kutumia wataalamu wa ndani na unatarajiwa kukamilika ndani ya mwaka mmoja.
“Mhe. Waziri Mkuu mradi huu umefikia asilimia 82 ya utekelezaji wake na utakamilkika katika muda ambao tumeupanga” amesema Twange.

Aidha amesema gharama ya utekelezaji wa mradi wa kituo cha kupokea na kupoza umeme umegarimu shilingi bilioni 27, ambapo mpaka sasa Serikali imetumia shilingi bilioni 15 na kazi zote za msingi zimekamilika na ujenzi unaendelea.
Mradi wa kituo cha kupokea na kupoza umeme cha Imalilo unatarajiwa kuboresha upatikanaji wa huduma ya umeme katika mikoa ya Simiyu, Mara na maeneo jirani.


More Stories
FCC yapongezwa kulinda walaji, kuchochea biashara
Waongezewa nguvu huduma za mama wajawazito Same
Wasusi watakiwa kutumia programu ya “Darling Hair” kujiimarisha