April 16, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Mbunge kuishawishi serikali kupata walimu shule wenye ulemavu

Na Esther Macha, Timesmajira Online, Chunya

MBUNGE wa Lupa, wilayani Chunya, mkoani Mbeya Masache Kasaka amesema kuwa kutokana na changamoto ya  uhaba wa walimu wa shule ya msingi kibaoni yenye watoto wenye ulemavu  analazimika kuishawishi  Serikali kuajiri wataalam wa lugha za harama ili kuwezesha kundi hilo kupata elimu.

Mbunge wa Lupa, wilayani Chunya, mkoani Mbeya Masache Kasaka

Kasaka amesema hayo  jana wakati akizungumza na waandishi wa habari ikiwa ni kutimiza mwaka mmoja tangu wananchi wampe ridhaa ya kuwatumikia na kuwawakilisha bungeni..

Amesem kuwa  licha ya Serikali kutenga fedha zaidi ya Sh 900  milioni  kwa ajili  ya ujenzi wa vyumba vya madarasa kwa shule za Sekondari wilayani humo bado kuna changamoto ya walimu wa lugha za  harama 

“Hii ni changamoto katika shule hii ya Kibaoni ni kubwa kutokana na ukubwa wa Wilaya yetu ,shule hii inahudumia watoto wenye ulemavu wa viungo,mtindio wa ubongo,watoto wenye ulemavu wa kusikia ,wilaya inafanya mikakati kupata walimu wa watoto wenye ulemavu wa kusikia”amesema  Mbunge huyo.

Masache amesema kuwa hawana walimu kwa ajili ya viziwi na kwamba kwa upande wa shule ya msingi  Lupa kuna shule moja ambayo sio maalum kwa ajili ya walemavu ila inatumika kwa eneo la Kipambawe kwani imeweza kusaidia kwani huko nyuma wazazi waliokuwa wakizaa watoto wenye ulemavu walikuwa wakiwaficha ndani uwepo wa shule umesaidia.

Aidha Mbunge huyo amesema kwamba uwepo wa shule hiyo umeweza kusaidia wazazi na walezi  walio wengi wameanza kuwatoa ndani  watoto wenye ulemavu ambao walikuwa wakificha wamepata mwamko wa  kuwapeleka shule .

“Hapa shule wanapewa chakula bure walau inasaidia wazazi na walezi kuwa na mwamko ,bado kuna shida ya walimu wa kuwahudumia hawa watoto kwani wanaowahudumia ni walimu wa kawaida tu sasa tunatamani ingekuwa rasmi kwa walemavu tu wapatikane walimu ambao wapo kwa ajili ya walemavu hawa walimu wanajua jinsi gani ya kuwalea watoto wenye ulemavu  inatakiwa kuwa mzazi kabisa,lakini kwa hawa walimu wa kwetu ambao wapo kwa ajili ya ajira mfano mtoto amejisaidia  inakuwa ngumu kwake”amesema  Masache.

Hata hivyo Masache amesema kwanza ilikuwa kuwatambua watoto wenye ulemavu katika wilaya ya Chunya kwanza na kwamba changamoto kubwa ilikuwa kutotangazwa ajira hivyo wataongea na halmasahauri kupata walimu ambao watajitolea kwa kuwapa posho kidogo wanakuwa kama wanajitolea.

“Mkakati wa muda mrefu ni kuiambia serikali inapotoa ajira kwa  walimu iangalie pia walimu kwa ajili ya kufundisha watoto wenye ulemavu hasa watoto wenye ulemavu wa kusikia ambapo kwa wilaya chunya hakuna walimu wa watoto wenye ulemavu wa kusikia.

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Chunya ,Saimon Mayeka amesema kuwa walilazimika kuanzisha shule hizo ambazo hazikuwa rasmi kwa ajili ya watoto wenye ulemau ili wazazi wapate msukumo wa kuwapeleka shule watoto wao,na kwamba kwa mwaka huu wanafikiria kutenga bajeti kutoka wizarani ili kusaidia shule hizo.

Aidha Mayeka alisema kutokana na uhitaji mkubwa kwa wilaya hiyo wameanza mikakati ya kuanzisha shule nyingine ya watoto wenye ulemavu katika Mji wa Makongolosi wilayani hapa .

“licha ya wizara pia kuweka bajeti kidogo ila upande wetu wa bajeti ya mkaa tumeongeza ushuru ili kuweza kuhudumia shule hizi fedha itatoka kwenye ushuru wa mkaa ,tuna kuni kubwa la watu wenye ulemau wa kusikia tunajipanga  kuwapata ili waende shule kwa kutumia bajeti yetu kwa kutafuta walimu ambao watasaidia kufundisha watoto hawa kwa kuwalipa posho kidogo”amesema Mayeka.