December 7, 2021

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

MATUKIO YALIYOSISIMUA

Mwendesha pikipiki Gilbert Delos Reyes mkazi wa Imus mjini Cavite, Ufilipino akiendesha pikipiki huku akiwa amempakiza mbele mbwa wake anayejulikana kwa jina la Bogie juzi. Haikujulikana mara moja anampeleka wapi mbwa huyo. (Picha na REUTERS).

Wakimbizi kutoka Ethiopia wakijaribu kumuwahi punda aliyeruka katika boti wakati wakivuka mto kutoka nchini humo kwenda kutafuta hifadhi kambi ya Hamdeyat iliyopo Sudan juzi. Maelfu ya raia wanaendelea kukimbia katika Jimbo la Tigray nchini Ethiopia kutokana na mgogoro mkubwa uliozuka tangu mwanzoni mwa mwezi Novemba, mwaka huu. (Picha na REUTERS).
Polisi wakikabiliana na watu ambao walikuwa wanalazimisha kwenda kuuona mwili wa marehemu Diego Maradona wakati taratibu za maziko zikiendelea mjini Buenos Aires, Argentina Novemba 26, 2020. (Picha na REUTERS).
Wafanyakazi wakiendelea kutoa taka katika Mto Yangtze uliopo mjini Yichang katika Jimbo la Hubei nchini China juzi.Shughuli za kila siku za binadamu zimekuwa miongoni mwa sababu ambazo zinachangia uchafuzi wa mazingira duniani. (Picha na AFP).
Picha iliyopigwa kwa ndege ndogo aina ya drone ikionyesha taswira ya barabara iliyopo katikati ya msitu mnene uliopo karibu na Kijiji cha Korytniki mkoani Podkarpacie Kusini Mashariki mwa Poland juzi. Licha ya msitu huo kufunga mara kwa mara kutokana na barafu nzito, barabara hiyo imeendelea kuwa tegemeo kwa wananchi wa kijiji hicho. (Picha na EPA-EFE).