April 28, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Majaliwa mgeni rasmi mashindano ya Sayansi,Ubunifu na Teknolojia

Na Joyce Kasiki, Timesmajira Online, Dodoma

WAZIRI Mkuu Kasim Majaliwa, leo anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika kilele cha Mashindano ya Kitaifa ya Sayansi ,Teknolojia na Ubunifu (MAKISATU) .

Akizungumza leo na waandishi wa habari katika Uwanja cha Jamhuri jijini Dodoma, ambako mashindano nayo yanafanyika tangu Mei 6, mwaka huu Mkurugenzi wa Sayansi,Teknolojia na Ubunifu Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia, Profesa Maulilio Kipanyula amesema, katika kilele cha mashindano hayo kutakuwa na utoaji wa tuzo kwa washindi wa bidhaa mbalimbali.

Profesa Kipanyula wamesema taasisi zipatazo 50 zimeshiriki, huku akiwasishi wananchi kujitokeza kwa wingi kushiriki katika mashindano nayo kuona na kununua bidhaa zilizotengenezwa na wabunifu wa mashindano hayo.

Profesa Kipanyula akizungumza na waandishi wa habari kuhusu kilele cha mashindano ya MAKISATU.

“Zipo bidhaa mbalimbali zenye kutatua changamoto katika jamii, nawasihi wananchi wajitokeze kwa wingi kuona ubunifu, lakini pia kununua bunifu ambazo nazo tayari zipo sokoni.” amesema Profesa Kipanyula