May 10, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Hassan Abbasi akizindua tamthilia mpya ya WE-MEN na Chaneli mpya ya TV3 katika Ukumbi wa Hyatti jijini Dar es salaam.

Serikali kuweka mifumo kulinda maslahi ya kazi za sanaa

Na Mwandishi Wetu, TimesMajira Online, Dar es Salaam

KATIBU Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Hassan Abbasi amesema  Serikali inaweka mifumo bora kwa ajili ya kuboresha kazi za sanaa na kulinda masalahi ya wasanii.

Dkt. Abbasi ameyasema hayo Mei 9, 2021 kwenye Iftar maalum iliyoandaliwa na Star Times kuzindua tamthilia mpya ya WE-MEN na Chaneli mpya ya TV3 katika Ukumbi wa Hyatti jijini Dar es salaam.

“Kazi za Wasanii wengi wa hapa nchini zinachezwa na kuangaliwa sana duniani lakini wamiliki wa kazi hizo hampati chochote” amesema Dkt. Abbasi.

Dkt. Abbasi amefafanua kuwa kupitia mwaka mpya wa fedha wa 2021/22  Serikali itakua na  kodi maalumu ya kutoza makampuni mbalimbali  yanayokuja nchini kwa ajili ya  kutumia ama kuuza kazi za wasanii ambayo  itamfaidisha msanii moja kwa moja.

Aidha  Katibu Mkuu Dkt.Abbasi amewasisitiza wasanii kufanya kazi bora kwasabau muziki, filamu na sanaa zima kwa ujumla duniani ipo katika ushindani mkubwa, hivyo wanapaswa kutengeneza kazi zenye kiwango cha hali ya juu kukidhi mahitaji na Soko Duniani.

Hata hivyo Dkt. Abbasi ameipongeza Kampuni hiyo kwa kuwekeza katika filamu za kitanzania na pia kwa kuanzisha Chaneli mpya ya TV3 itakayokuwa inarusha mashindano ya EURO 2020 ambayo uchambuzi  wa mashindano hayo utakuwa ukifanyika kwa lugha ya kiswahili.

“Nawashukuru Star Times kwa kazi kubwa mnayoifanya Tanzania, mmetafuta soko la kazi zetu za sanaa hongereni sana” Dkt. Abbasi.