May 10, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Kikwete : Mabadiliko ya Tabianchi bado changamoto nchini

Na Mwandishi wetu Timesmajira online

RAIS Mstaafu wa Awamu ya nne Dkt Jakaya Kikwete amesema mabadiliko ya tabia ya nchi bado ni chagamoto na yamekuwa yakiathiri zaidi sekta ya maji hivyo jitihada muhimu zinaitajika.

Dkt Jakaya Kikwete ametoa kauli hiyo Jijini Dar es salaam wakati akifungua Maadhimisho ya miaka 50 ya Chuo Cha maji ambayo yalienda sambamba na kongamano la tatu la kitaifa la kisayansi ambalo limeandaliwa na chuo hicho.

Amesema katika matatizo ya athari ya mabadiliko ya tabianchi sekta inayoathirika sana ni ya maji ambayo imekuwa na athari ambazo zinaonekana na kusababisha ukame

“Mabadiliko ya tabia ya nchi yanasababishwa na kujirudia mara Kwa mara Kwa ukame pia mabadiliko haya yamekuwa ni ya uhalisia zaidi kutokana kuathiri maeneo mbalimbali ya nchi na kusababisha madhara makubwa.

“Sisi Kwa mkoa wa Pwani tumekuwa tukichimba visima lakini Kwa Sasa maji ambayo yamekuwa yakitoka ni maji ya chumvi kabisa haya yote yanatokana na matatizo ya mabadiliko ya tabianchi .amesisitiza Dkt Jakaya

Aidha amesema mabadiliko hayo ya tabia ya nchi yamekuwa yakisababishwa na kuongezeka kwa hewa ya ukaa pamoja joto.

“Kiukweli tunamazingira magumu sana nafurahi kuwa suala hili pia mtaweza kulijadili kwani sekta ya maji ndio imekuwa ikiathirika zaidi “amesema Dkt Jakaya

Pia kupitia mkutano huo Dkt Jakaya Kikwete amekitaka chuo cha Maji Dar es Salaam kuhakikisha kinazalisha Wataalam watakaoweza kupambana katika soko la ajira na kutoa suluhu kwa changamoto zinazoikabili sekta ya maji nchini.

Dkt Jakaya aliutaka uongozi wa chuo hicho cha Maji Dar es Salaam kutumia vema fedha zinatolewa na Serikali ili kutimiza malengo yaliyokusudiwa katika kumtua Mama ndoo kichwani.

“Ombi langu fedha mnazopata ni nyingi zitumieni vizuri na zitumike Kwa malengo yaliokusudiwa “alisema Dkt Jakaya

Vilevile amempongeza Waziri wa maji Jumaa Uweso Kwa kazi kubwa ambayo akiifanya ambapo ameomba Uongozi wa chuo hicho kumuunga mkono hususani katika matumizi ya fedha .

Kwa upande wake Mkuu wa chuo Cha maji Dkt Adam Karia amesema Chuo Cha maji ni muhimili katika sekta ya maji .

Dkt Karia amesema Chuo hicho kimekuwa na majukumu ya kutoa mafunzo, kufanya tafiti pamoja na kutoa ushauri na Kwa sasa inamatawi matatu.

Aidha Dkt Karia ameishukuru Serikali kwa kuendelea kutenga fedha kwa ajilj ya chuo hicho ili kukiwezesha kufanya maboresho mbalimbali.