August 7, 2026

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Jeshi la Polisi latoa elimu kwa wananchi nanenane.

Na Mwandishi wetu,Timesmajira

KAMANDA wa Polisi Mkoa wa Dodoma, ACP Gallus Hyera amesema Jeshi hilo
linaendelea kushirikiana na waganga wa tiba asili katika kutoa elimu kwa jamii, huku likiwataka kuzingatia sheria za nchi na kutoa taarifa kwa vyombo vya usalama wanapobaini wahalifu wanaotafuta huduma kwa lengo la kuficha au kuendeleza vitendo vya uhalifu.

ACP Hyera ameyabainisha hayo katika maonesho ya Kilimo nane nane yanayoendelea Jijini Dodoma ambapo kupitia maonesho hayo wakitoa elimu kwa wananchi kuhusu huduma mbalimbali zinazotolewa na jeshi hilo pamoja na kuhamasisha ushirikiano katika kudumisha amani na usalama.

“Jeshi la Polisi
limeundwa kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Sheria ya Jeshi la Polisi na Polisi Wasaidizi, likiwa na jukumu la kusimamia utekelezaji wa sheria, kulinda amani na usalama, kupeleleza makosa ya jinai, kukamata wahalifu na kulinda raia pamoja na mali zao”amesema

Aidha Jeshi la Polisi Mkoa wa Dodoma linaendelea kutekeleza majukumu yake kupitia doria, misako na operesheni mbalimbali, huku likiimarisha ulinzi katika viwanja vya maonesho ili kuhakikisha usalama wa washiriki na wageni wote.

Aliongeza kuwa elimu hiyo inalenga kuwajengea wananchi uelewa wa huduma zinazopatikana katika vituo vya polisi ili iwe rahisi kwao kupata huduma wanapozihitaji.
Pia alieleza kuwa

Aidha ametoa wito kwa wananchi kuendelea kutembelea banda la Jeshi la Polisi katika maonesho hayo ili kupata elimu kuhusu huduma mbalimbali zinazotolewa na jeshi hilo na kushiriki katika juhudi za kulinda amani, utulivu na usalama nchini.