October 20, 2021

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Haji Manara ahamia Yanga na Familia yake

Na Mwandishi Wetu, Timesmajira Online

Aliyekuwa Msemaji wa klabu ya Simba, Haji Manara

ametangaza rasmi kujiunga na Yanga jioni hii Jijini

Dar es salaam, na pia amesema amehamia klabu hiyo

pamoja na Familia yake.

Akizungumza mara baada ya kutambuishwa rasmi kwenye

Hotel ya Serena Jijini Dar es Salaam, Manara

amesema, anakwenda Yanga kutokana na kuwa na

viongozi watakaompa nafasi ya kuwasaidia.

“Nakwenda Yanga kwa sababu ina viongozi watakaonipa

nafasi ya kuwasaidia, nilibanwa mno, nilidhihakiwa

mno, sijawahi kuwa na matatizo na Simba,” amesema

Manara.