Na Mwandishi wetu, TimesMajira Online
KUELEKEA msimu wa 10 wa mashindano ya Mbeya Betika Tulia Marathon, spika mstaafu wa Bunge la Tanzania, Dkt.Tulia Ackson amesema amejiandaa kikamilifu kushiriki mbio za kilomita 42 zitakazofanyika leo Mei 16, 2026 jijini Mbeya.
Dkt. Tulia amesema hayo wakati akifungua rasmi mbio za uwanjani za Mbeya Betika Tulia Marathon zilizofanyika katika Sokoine Stadium.

“Siku ya kwanza ya mashindano haya inahusisha mbio za mita 100 hadi 1,500. ……hizi ni mbio za kipekee nchini zinazowaandaa wanariadha kwa mashindano ya kimataifa ya uwanjani, huku kesho kukiwa na mbio nyingi zaidi,” amesema Dkt. Tulia.
Amesema washiriki wameonyesha ushindani mkubwa na wengi wao wamejiandaa vizuri, jambo lililochangia baadhi ya mashindano kukamilika kwa mafanikio makubwa.
Afisa mawasiliano na uhusiano wa Tulia Trust, Joshua Mwakanolo, amesema mashindano ya mwaka huu yameweka rekodi mpya ya ushiriki kutokana na mwitikio mkubwa wa wanariadha na wananchi ukilinganisha na misimu iliyopita.

Amesema mbio za kilomita tano zimeendelea kuwa kivutio kikubwa kwa washiriki wengi zaidi, huku zikiandika rekodi mpya ya ushiriki katika mashindano hayo.
Mwakanolo amesema ratiba ya mashindano ya mwaka huu pia imejumuisha mbio za watoto pamoja na mashindano ya kuruka, yakilenga kukuza vipaji vya vijana na watoto katika mchezo wa riadha nchini.

More Stories
Kikwete: Nidhamu na Uadilifu ni msingi wa maendeleo ya taifa
Madaktari Mloganzila wanufaika na mafunzo maalum ya tiba za mifupa
Mwanasheria Mkuu wa Serikali,Simbu kung’ara Mbio za Wakili Marathon 2026