Na Yusuph Mussa, Timesmajiraonline,Dodoma
MKURUGENZI Mtendaji wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo nchini (TADB), Frank Nyabundege amesema mikopo ya sh. bilioni 692 imetolewa na benki hiyo kwenda benki 21 nchini ili ziweze kuwakopesha wakulima wadogo wadogo wasio na dhamana, na wameweza kuwafikia wakulima 657,000
Na hiyo imewezekana baada ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kuiwezesha benki hiyo, kwani wakati anaingia madarakani Machi 19, 2021, benki hiyo ilikuwa na mtaji wa sh. bilioni 60, lakini katika kipindi chake cha miaka mitano sasa, benki hiyo ina mtaji wa sh. bilioni 452.
Ameyasema hayo Agosti 8, 2026 mbele ya Rais Dkt. Samia kwenye kilele cha Maadhimisho ya Maonesho ya Kilimo (Nanenane) ya Kitaifa yaliyofanyika Viwanja vya John Samwel Malecela jijini Dodoma

“Benki hii imekuwa kinara kwenye kutoa mikopo kwenye Sekta ya Kilimo sana sana kwenye awamu yako ukiwa Kiongozi wetu. Ulipoingia madarakani mwaka 2021, benki ilikuwa na mtaji wa sh. bilioni 60 pekee, lakini kwa hii miaka michache umeiongezea sh. bilioni 392 sawa na asilimia 86.7, na kufikia sh. bilioni 452. Na hii sasa imeifanya benki kutoa mikopo kwa kasi zaidi na kuweza kukuza mikopo, na takribani ya asilimia 84 ya mikopo tuliyoitoa ya sh. trilioni 1.32 imetolewa kwenye kipindi chako cha miaka mitano.
“Na hii ni kwa sababu umeweza kutupatia mtaji kama nilivyosema, umeweza kututafutia fedha kwa wafadhili mbalimbali sh. bilioni 591 na kuifanya benki yetu kuwa kinara, na hivyo kutufanya kuwa na nguvu kubwa, na kutoa mikopo kwa taasisi nyingine ili ziweze kuwafikia wakulima zaidi ya sh. bilioni 692 zimetolewa na benki kwenda benki 21 nchini ili ziweze kuwakopesha wakulima wadogo wadogo wasio na dhamana, na wameweza kuwafikia wakulima 657,000. Hadi sasa tumewafikia wakulima milioni 2.6, na kufadhili miradi 862″amesema.
Nyabundege amesema kwa umahiri walioufanya, Benki ya TADB imepokea Tuzo ya Benki Bora katika kutoa Suluhisho la Ufadhili wa Kilimo nchini Tanzania iliyotolewa na Clobal Brand Awards.

“Kutokana na jinsi tulivyokuwa tukifanya, na brnki hii kukuwa kwa kasi hadi wenzetu wa nje wakitushangaa walipokuwa wakitufanyia tathmini, nipende kukufahsmisha mheshimiwa Rais, Benki ya TADB tumepata heshima ya kutunukiwa Clobal Brand Awards.2026 ya kimataifa. Imetunukiwa Award hii kama Benki Bora yenye Suluhisho bora la kifedha kwenye Sekta ya Kilimo nchini Tanzania.
“Walikuja na kuona benki hii, sio tu kwamba tunatoa mikopo peke yetu, bali tunawapatia na benki nyingine ili waweze kuwapatia mikopo wakulima wote nchini kwa wingi zaidi, na wakaona tukitoa masuluhisho hasa kwa mabadiliko ya Tabianchi, na wakaona tunastahili.Na Tuzo hii ni benki moja tu Afrika nchini Tanzania tumeweza kuipata”amesema Nyabundege.




More Stories
Wananchi watakiwa kutunza,kulinda barabara
Self Microfinance kutekeleza Dira 2050 kupitia mikopo
Ndejembi amtaka Mkandarasi kuongeza kasi ujenzi wa Barabara ya Kahama