May 13, 2026

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Baraza la Madiwani Nkasi limemfukuza kazi mtumishi wa afya kwa utovu wa nidhamu

Na Israel Mwaisaka, Rukwa

‎BARAZA la Madiwani halmashauri ya wilaya Nkasi mkoani Rukwa imemfukuza kazi mtumishi wa idara ya afya Kituo Cha afya Kabwe Zakaria  Petro Mrisho kwa makosa mbalimbali ikiwemo ya uwizi wa vifaa  tiba na dawa.

‎Akitoa taarifa hiyo leo Mei 8,2026 kwenye kikao Cha Cha robo ya tatu kwa mwaka wa Fedha 2025-2026  Mwenyekiti wa halmashauri Richard Masai amesema kuwa baraza lilijigeuza na kuwa kamati ya maadili na kupitia shauri la mtumishi huyo na kumkuta na hatia na kufikia uamuzi wa kumfukuza kazi.

‎Alisema kuwa mtumishi huyo wa afya aliyeajiliwa Novemba 21,2024  amekuwa akituhumiwa kwa muda mrefu kuhusika na upotevu wa vifaa tiba na dawa na kuwa uchunguzi uliandaliwa na taarifa ya uchunguzi huo ilibainisha mtumishi huyo kuhusika moja kwa moja na upotevu wa mali hizo za Serikali.

‎Mwenyekiti huyo wa halmashauri alifafanua kuwa licha ya taarifa ya uchunguzi pia kamati ya fedha nayo ilifanya uchunguzi wake na bila ya kuacha shaka yoyote walimkuta mtumishi huyo na hatia ya uwizi.

‎Hivyo kwa kupitia taratibu mbalimbali za kiutumishi zilizokuwa zimefuatwa Baraza hilo limefikia hatua ya kumfukuza kazi rasmi mtumishi huyo na kuwa kuanzia leo Mei 8,2026 Mtu huyo siyo mtumishi tena wa serikali

‎Pia amedai kuwa katika kikao hicho wamewathibitisha Watumishi  Wanne wa halmashauri hiyo kuwa wakuu wa idara na vitengo ambao ni Steward vidoga kuwa Mkuu wa divisheni ya mipango na uratibu,Silima Milao  Divisheni ya fedha na uchumi,Barnaba Amon Mhalila Divisheni ya Viwanda na biashara na Rainel Mwenda Mkuu wa Divisheni ya utawala na rasilimali Watu.

‎Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya Wilaya Afraha Hassan kwa upande wake aliwataka watendaji kuendelea kusimamia maelekezo yaliyotolewa katika Baraza hilo kwa lengo la kuhakikisha wanayafikia malengo ya kuwaletea maendeleo Wananchi

‎Na alidai kuwa kwa Sasa kazi kubwa iliyopo mbele Yao ni kukabiliana na changamoto ya uhaba wa madawati ambapo kwa shule za msingi Kuna uhaba wa madawati 21,088 na sekondari 15,000 na kuwa ili kufikia lengo hilo inahitajika Bil.3.3 na kuwa ili kupunguza gharama hizo wataendelea kuwasiliana na TFS na TAWA kwa lengo la kupata mbao ili kutengeneza madawati hayo.