April 26, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Barakah the Prince mbioni kuachia ngoma mpya

Na Mwandishi Wetu, Timesmajira Online

MSANII wa muziki wa Bongo fleva, Barakah the Prince amesema yupo mbioni kuachia ngoma yake mpya kwa ajili ya kuwapa raha mashabiki zake.

Akiweka wazi hilo kupitia IG yake Baraka amesema, ngoma hiyo itakuwa ya pili baada ya ile ya awali aliyoiachia hivi karibuni.

“Nafikiri ni muda mzuri sasa wa kuachia wimbo mwingine mpya, kwa hiyo fuatilia channel yangu ya Youtube kuanzia sasa,” amesema Baraka.