April 25, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Wizara ya Maliasili na Utalii yapokea magari kumi kutoka UNDP

Na Mwandishi wetu, TimesMajira Online, DSM

Wizara ya Maliasili na Utalii imekabidhiwa  magari kumi kutoka  Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Maendeleo (UNDP) kwa ajili ya kuongeza nguvu katika mapambano dhidi ya ujangili wa wanyamapori.

Akizungumza leo Jijini Dar es Salaam wakati wa hafla fupi ya kukabidhiwa magari hayo,  Katibu Mkuu wa  Maliasili na Utalii , Prof. Eliamani Sedoyeka amesema Magari hayo yanakwenda kwenye kaya 10 tofauti tofauti kwa  lengo la kuhakikisha kuwa  rasilimali za wanyamapori  zinalindwa kikamilifu.

“Nchi yetu ipo katika mapambano makali dhidi ya ujangili na  sisi kama wizara ya maliasili tuna jukumu la kuhakikisha  rasilimali zetu zinaendelea kutumikakwa ajili  ya kizazi cha sasa  na vizazi vijavyo”

Amesema Prof. Sedoyeka  Amesisitiza kuwa katika jitihada za kupambana na ujangili,  Wizara imeendelea kushirikiana na wadau wa ndani na nje ya nchi ikiwemo  UNDP, 

 “UNDP imetusaidia katika kuijengea  uwezo  timu yetu pamoja na kutuongezea vitendea kazi ambapo leo hii wametukabidhi magari 10 kwa ajili ya  mapambano hayo”

Kutokana na jitihada hizo,  Prof. Sedoyeka amesema odadi ya wanyama  wakubwa kama vile  tembo ba faru  waliokuwa  wakipungua kutokana na tatizo la ujangili  wameanza kuongezeka kwa kasi.

Kwa upande wake Mwakilishi Mkazi wa UNDP Tanzania,  Christine Musisi amesema kumekuwa na ushirikiano na Wizara ya Maliasili na Utalii kwa kipindi cha muda mrefu na hivyo  wamekuwa wakivutiwa na juhudi zinazofanywa na Wizara hiyo katika mapambano dhidi ya  ujangili wa wanyamapori 

” Tumeendelea kushirikiana na Wizara kwa kuwapatia vitendea kazi, kuwajengea uwezo watumishi na kupitia jitihada hizo idadi ya wanyama kama vile tembo imeongezeka maradufu,”alisema Mwakilishi wa UNDP

Musisi Mwakilishi huyo wa UNDP amesisitiza kuwa UNDP  itaendelea kuwa mdau mkubwa  wa uhifadhi kwa kuhakikisha kuwa wanyamapori wa Tanzania  wanaendelea kuwa salama kwa ajili ya manufaa makubwa ta  jamii na uchumi wa nchi.

Katibu Mkuu wa Maliasili na Utalii, Prof. Eliamani Sedoyeka (kushoto) akikata utepe pamoja na Mwakilishi Mkazi wa UNDP, Christine Musisi ikiwa ni ishara ya makabidhiano ya magari 10 kutoka UNDP wakati wa hafla fupi ya makabidhiano ya magari hayo iliyofanyika kwenye Ofisi za Wizara ya Maliasili na utalii Jjini Dar es Salaam.

Katibu Mkuu wa Maliasili na Utalii, Prof. Eliamani Sedoyeka (kulia) akipokea Mkataba wa Makabidhiano ya Magari 10 Kutoka Kwa Mwakilishi Mkazi wa UNDP nchini, Christine Musisi wakati wa Hafla fupi ya Makabidhiano ya Magari hayo yaliyotolewa kwa ajili ya mapambano dhidi ya ujangili leo Jijini Dar es Salaam.
Muonekano wa baadhi ya Magari yaliyokabidhiwa na UNDP kwa Wizara ya Maliasili na Utalii kwa ajili ya kusaidia mapambano dhidi ya ujangili leo jijini Dar eS Salaam.

Katibu Mkuu wa Maliasili na Utalii, Prof. Eliamani Sedoyeka akiendesha moja ya gari kati ya 10 yaliyokabidhiwa na UNDP kwa ajili ya mapambano dhidi ya ujangili leo jijini Dar es Salaam.
Mwakilishi Mkazi wa UNDP, Christine Musisi akizungumza wakati wa Hafla fupi ya Makabidhiano ya Magari 10 kutoka UNDP kwaajili ya kukabiriana na ujangili ambapo amesema UNDP nchini Tanzania itaendelea kushirikiana na serikali katika suala zima la kukabiriana na ujangili nchini.
Mkurugenzi wa Idara ya Wanyamapori, Dkt. Maurus Msuha akizungumza kabla ya kumkaribisha Katibu Mkuu wa Maliasili na Utalii, Prof. Eliamani Sedoyeka kuzungumza wakati wa hafla fupi wa makabidhiano ya Magari 10 kutoka UNDP kwa ajili ya mapambano dhidi ya ujangili iliyofanyika leo jijini Dar eS Salaam.