October 20, 2021

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Wiki ya Mwananchi kuanza rasmi Agosti 22, Visiwani Zanzibar

Na Mwandishi Wetu, Timesmajira Online

KLABU ya Yanga inatarajia kuzindua rasmi wiki ya Mwananchi Agosti 22 mwaka huu viziwani Zanzibar kwa ajii ya kuelekea kwenye kilele cha wiki hiyo itakayofayika Agosti 28 mwaka huu, kwenye dimba la Mkapa.

Akizungumzia hilo leo, Mwenyekiti wa Kamati ya Hamasa na Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Yanga, Suma Mwaitenda amesema Wiki ya Mwananchi inaashiria mambo ya fuatayo.

“Kumalizika kwa msimu uliopita 2020/21 na kuanza kwa msimu mpya 2021/22, Kutambulisha wachezaji na benchi la ufundi kuelekea msimu mpya. Kutambulisha wachezaji wa timu ya vijana na timu ya wanawake.
Kuzindua jezi kwa ajili ya msimu mpya wa 2021/22.

Hata hivyo, Kwenye wiki ya Mwananchi kutakuwa na shughuli za kurejesha kwa jamii kwa kutoa huduma ikiwa ni pamoja na kuchangia damu, kufanya usafi na kutoa misaada kwa wasiojiweza.