May 3, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

WCF yaelimisha wafanyakazi maonesho ya madini Geita

 NA K-VIS BLOG, GEITA

MFUKO wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF) umewata wadau na wananchi wanaotembelea Maonesho ya 6 ya Teknolojia ya Madini yanayofanyika viwanja vya Bombambili eneo la EPZ Mjini Geita, kufika kwenye banda la Mfuko huo ili kupata taarifa ya huduma zitolewazo na Mfuko lakini pia elimu ya fidia kwa wafanyakazi.

Maonesho hayo yaliyofunguliwa rasmi na Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Doto Biteko yamewaleta pamoja waoneshaji wapatao 400 ambapo WCF ni miongoni mwa taasisi za umma zinazoshiriki kwa lengo la kuwahudumia washiriki na wananchi wanaotembelea maonesho hayo.

Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF) ni Taasisi ya Hifadhi ya Jamii iliyoundwa kwa mujibu wa Kifungu cha 5 cha Sheria ya Fidia kwa Wafanyakazi [Sura 263 marejeo ya mwaka 2015] na inahusu waajiri na waajiriwa wote Tanzania Bara. Ambapo lengo la kuanzishwa kwa Mfuko huu ni kushughulikia masuala ya Fidia kwa Wafanyakazi waliopo katika sekta ya umma na binafsi ambao wataumia, kuugua ama kufariki kutokana na kazi wanazozifanya kwa mujibu wa mikataba ya ajira zao.

Pamoja na kupatiwa elimu ya fidia kwa wafanyakazi mwananchi akifika kwenye banda la WCF pia atapata taarifa kuhusu Mafao saba yatolewayo na Mfuko, ambayo ni pamoja na Huduma ya matibabu, Malipo ya ulemavu wa muda, Malipo ya ulemavu wa kudumu, Malipo kwa anayemhudumia mgonjwa, Huduma za utengemao, Msaada wa mazishi na Malipo kwa wategemezi endapo mfanyakazi atafariki.

Dhima ya WCF ni kupunguza athari za kijamii na kiuchumi za majanga yatokanayo na kazi kwa wafanyakazi, familia zao na waajiri kwa kutoa fidia stahiki, kwa usawa, uendelevu na ufanisi.

Kwa mujibu wa Sheria ya Fidia kwa Wafanyakazi, mwajiri yoyote Tanzania Bara anawajibika kujisajili katika Mfuko na kwa sasa huduma zimeboreshwa zaidi ambapo mwajiri anaweza kujisajili katika Mfuko kwa njia ya mtandao (portal.wcf.go.tz) au kwakujaza Fomu za usajili (WCR-1 na WCR-2) na kuziwasilisha kwenye ofisi ya Mfuko iliyopo karibu nae au ofisi za idara ya kazi.

Maonesho hayo ya sita ya madini yamebeba kauli mbiu isemayo “Matumizi ya teknolojia sahihi katika kuinua wachimbaji wadogo kiuchumi na kuhifadhi mazingira.” Yanatarajiwa kufikia kilele Septemba 30, 20