Na Mwandishi Wetu, Timesmajira Online
WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Ajira na Mahusiano, Deus Sangu, ameipongeza kampuni ya Yas kwa ushiriki wake katika Maonesho ya Nanenane ya Mkoa wa Lindi.
Amesema, mchango wa sekta binafsi unaendelea kuwa nguzo muhimu katika kuharakisha maendeleo ya kilimo na mageuzi ya kidijitali nchini.
Sangu ameyasema hayo alipotembelea Banda la Yas na kupokea maelezo kuhusu huduma za mawasiliano na kifedha kidijitali zinazotolewa na Yas na Mixx.
Kwa upande wake, Meneja wa Biashara na Masoko wa Yas – Kanda ya Pwani Kusini, George Msofe, amesema maonesho hayo yameendelea kuwa jukwaa muhimu la kuwafikia wakulima na wananchi kwa kuwaelimisha kuhusu suluhisho za kidijitali zinazorahisisha mawasiliano, malipo na ukuaji wa biashara.
“Yas itaendelea kushirikiana na wadau mbalimbali kuhakikisha teknolojia na huduma za kidijitali zinawafikia Watanzania wengi zaidi, hususan wakulima.
Lengo likiwa kuwawezesha kuongeza tija na kushiriki kikamilifu katika uchumi wa kidijitali,” alisema Msofe.

More Stories
Nanauka apongeza Kariakoo Kwa kuwezesha vijana Kibiashara
Uzalishaji mbegu bora waongezeka kwa asilimia 55 nchini
Pinda:Vijana JKT tumieni muda vizuri