May 8, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Waziri Nape kuja na Mwarobaini Ajali za Wanahabari kwenye misafara ya viongozi

Na Mwandishi wetu, TimesMajira Online

Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye ameliagiza Jeshi la Polisi kutoa taarifa za matukio yote ya ajali za barabarani kwenye misafara ya viongozi nchini ambayo yanachukua maisha ya wana tasnia hiyo ili zipitiwe na kujua ni kwanini zinawagusa wanahabari ili kuchukua hatua ya kuweka itifaki nzuri itakayowalinda wanahabari wanapotimiza wajibu wao kwenye misafara ya viongozi.

Amesema hayo wakati akitoa pole kwenye hafla ya kuaga miili ya wanahabari watanoiliyofanyika mkoani Mwanza.

“Nilipokuwa nakuja huku wakubwa wangu wamenielekeza kuwa nifuatilie hili la ajali kwenye misafara ya viongozi,kwani waathirika wamekuwa ni waandishi wa habari,lazima tujue chanzo ni nini,”amesema.

Waziri Nape amesema jambo hilo watalisimamia kuhakikisha kuwa waandishi wa habari wote wanakuwa salama kwenye kutimiza majukumu yao.

Aidha alimaliza kwa kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa maisha ya marehemu hao watano na amewasihi watu wote waendelee kuwakumbuka kwa kazi zao walizokuwa wakizifanya.