Na Mwandishiwetu,Timesmajira.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Mahmoud Thabit Kombo amewasili jijini Djibouti, Jamhuri ya Djibouti kwaajili ya kumuwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzani Dkt. Samia Suluhu Hassan kwenye sherehe za Uapisho wa Rais Mteule wa nchi hiyo, Ismaïl Omar Guelleh.
Kombo amewasili jijini hapo Mei 08, 2026 kupitia Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Djibouti-Ambouli na kupokelewa na Waziri wa Bajeti wa nchi hiyo Isman Ibrahim Robleh.

Waziri Kombo anatarajiwa kushiriki katika sherehe hizo za uapisho wa Rais Mteule wa Jamhuri ya Djibouti,Ismail Omar Guelleh zinazotarajiwa kufanyika jijini hapa leo Mei 09, 2026 katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Djibouti akimuwakilisha Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Rais Mteule wa Djibouti Ismaïl Omar Guelleh amechaguliwa kuongoza nchi hiyo kwa muhula wa sita mfululizo kufuatia ushindi wa kishindo kwenye uchaguzi mkuu uliofanyika Tarehe 10 Aprili, 2026 nchini humo.

More Stories
Milioni 299 kutumika kujenga ofisi za kata
Mtanda asisitiza matumizi ya takwimu serikalini
Maofisa Habari watakiwa kuhabarisha taarifa sahihi