May 1, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Waziri Bashungwa kutembelea miradi Chita JKT

MAKAMU Mwenyekiti  wa Kamati ya Kilimo mkakati,Mifugo na Uvuvi wa Jeshi la Kujenga Taifa ambaye pia ni Mkurugenzi wa Kilimo,Mifugo na Uvuvi wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT)  Kanali Peter Lushika akionyesha namna vifaranga vya samaki vinavyototoleshwa ambayo ni moja ya shuguli zinazofanywa na JKT katika kikosi 837 Chita KJ

Na Joyce Kasiki,Timesmajira online,Chita-Kilombero

WAZIRI wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Innocent Bashungwa leo anafanya ziara katika kikosi cha 837 Chita Kilombero mkoani Morogoro kwa ajili ya kukagua miradi mbalimbali ikiwemo ya Kilimo na ufugaji inayofanywa na Jeshi la Kujenga Taifa katika kikosi hicho.

Akizungumza na waandishi wa habari kikosini hapo Makamu Mwenyekjiti  wa Kamati ya Kilimo mkakati,Mifugo na Uvuvi wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT)  Kanali Peter Lushika,amesema lengo la ziara hiyo ni kujionea shughuli zinazofanywa na JKT kikosini hapo ambapo pia watapokea maelekezo yake ili kuboresha utendaji wa miradi mbalimbali wanayoitekeleza.

Aidha Kanali Lushika ambaye pia ni Mkurugenzi wa Kilimo,Mifugo na Uvuvi JKT  amesema JKT inatekeleza miradi hiyo kwa weledi huku akisisitiza wanaendelea na kilimo cha mpunga katika shamba la Mngeta lililopo  Mlimba mkoani Morogoro.

Naye Mkuu wa kikosi hicho Luteni Kanali Emmanuel Kukula amesema katika kikosi hicho kwa kushirikiana na Vijana wa JKT wanafanya  shughuli za ufugaji wa samaki ikiwemo kutotolesha vifaranga vya samaki ambapo vijana  wanafundishwa shughuli mbalimbali zikiwemo za ufugaji wa samaki kwa kugawanywa katika vikundi vidogo ili waweze kuelewa kile wanachofundishwa.

Mkuu wa kikosi 837 Chita KJ Kanali Emmanuel Kukula