May 22, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Pamba Fc yapongezwa kupanda ligi kuu bara

Na Raphael Okello, Timesmajiraonline,Mwanza.

WAPENZI soka  mkoani Mwanza wamepongeza timu ya Pamba Fc kupanda ligi kuu bara msimu ujao wa mwaka 2024/ 2025.

Wakipokea timu hiyo ya Pamba Fc leo Aprili 30,2024 kutoka jijini Arusha wapenzi wa soka  jijini hapa walijitokeza kwa wingi huku wakimwagia sifa uongozi wa timu na wachezaji wake.

Pia wamepongeza viongozi wa halmashauri ya jiji la Mwanza,Mkuu wa Mkoa huo Said Ntanda pamoja na aliyekuwa Mkuu wa Mkoa huo Amos  Makalla, wananchi na wafanyabiashara, kwa ujumla kwa kuunga mkono timu hiyo.

Wakizungumza na mwandishi wa habari washabiki wa mchezo wa mpira wa miguu waliwamwagia pongezi, aliyekuwa mkuu wa mkoa huo, Amos Makalla ambaye hivi karibuni aliteuliwa na Rais Dkt. Samia kuwa Katibu wa itikadi ,mafunzo na uenezi wa CCM taifa.

Wamesema kuwa Makalla alichangia mafanikio ya Timu ya Pamba Fc na kutoa rai kwa mkuu wa mkoa wa sasa Saidi Ntanda kuendeleza juhudi hizo.

Aidha walimtaja  aliyekuwa mkurugenzi wa jiji la Mwanza, Aron Kagurumjuli kwa ushirikiano kati yake na Pamba Fc  kwa kuhakikisha timu hiyo inafanya vizuri na na kupanda ligi kuu toka ligi daraja la kwanza.

Afisa habari wa Timu ya ya Pamba Fc  Martin Mgono Sawema  amesema kuwa Mafanikio yote yametokana na nia pamoja na Dhamira ya Mkoa wa Mwanza kutaka kuwa na timu inayocheza ligi kuu

Amesema mkoa wa Mwanza utahakikisha kuwa Pamba inaingia katika Ligi kuu kwa kishindo na kuleta mwamko wa pekee katika ligi kuu Bara, 2024/2025.