May 15, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Wataalamu wa dawa za usingizi na ganzi wanolewa

Na Esther Macha,TimesmajiraOnline,Mbeya

TIMU ya watalaamu wautoaji salama wa dawa za usingizi na ganzi wa Hospitali ya Rufaa kanda ya Mbeya wamejengewa uwezo na kubadilishana ujuzi wa matumizi ya vifaa tiba vipya vya kisasa ili kuwaongezea ufanisi katika utoaji huduma za matibabu kwa wagonjwa .

Akizungumza mara baada ya mafunzo hayo leo Mtaalamu wa vifaa tiba,Rodgers Nyangeri amesema kuwa amefika katika hospitali ya Rufaa kanda ya Mbeya kitengo cha wazazi kutoa mafunzo ili waweze kutumia vifaa tiba hivyo vizuri ambavyo ni vya teknolojia ya kisasa wakati wa kutoa huduma za dawa ya usingizi na ganzi kipindi cha upasuaji .

“Siku ya leo tupo hapa ili kutoa mafunzo kwa wataalam ili waweze kutumia vifaa hivyo vizuri vya kisasa wakati wa kutoa dawa za usingizi na ganzi lakini pia nishukuru serikali chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kutoa vifaa hivyo vya kisasa ambavyo vitakuwa msaada mkubwa kwa watalaam hao “amesema Nyangeri.

Aidha amesema mafunzo hayo yatakuwa msaada kwa wataalam pindi wagonjwa wanapolazwa kujua mgonjwa anahitaji huduma gani na mgonjwa aliyelazwa kupata huduma nzuri zaidi na kama kukitokea shida yeyote wakati mgonjwa akipatiwa dawa ya usingizi na ganzi mashine zinaweza kutoa taarifa kwa mtalaam mgonjwa ana shida fulani ili kusaidia kupewa dawa nyingine kikamilifu.

Sharifa Nyambwila ni Mtaalam wa dawa za usingizi na Ganzi hospitali ya Rufaa kanda ya Mbeya amesema kuwa amepata mafunzo ya kutumia mashine kwa ajili ya kutoa huduma kwa wagonjwa wa hospitali ya rufaa na kushukuru kuletewa mashine hizo kwani zitawawezesha kupata uwezo zaidi na kutoa huduma nzuri kwa wagonjwa na kuleta tija nzuri kwa wagonjwa.

“Kupitia mafunzo haya ya yameniongozea ujuzi na uwezo wa kutoa huduma nzuri wa dawa za usingizi kwa wagonjwa wetu ,lakini nashukuru pia serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Dkt, Samia Suluhu Hassan kutuwezesha kupata vifaa tiba vipya vya kisasa ambvavyo vitasaidia kutoa huduma nzuri kwa wagonjwa”amesema Mtaalam huyo.

Mtaalam mwingine wa dawa za usingizi na Ganzi hospitali ya rufaa kanda ya Mbeya,Guydon Makulila amesema Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan ameamua watanzania wapate huduma kwa ufasaha na usalama zaidi ndo sababu kuu ya kupatiwa mafunzo hayo ili kuendeleza afya kwa ajili ya kutoa huduma nzuri kwa wagonjwa .

“Ndiyo maana hii leo tuna hizi mashine mpya za kisasa katika hospitali yetu ya rufaa kanda kitengo cha wazazi Meta kuhakikisha akina mama wanaokuja kupata huduma ya upasuaji wapate huduma na zilizo bora zaidi katika kuokoa maisha ya mama na mtoto ,sisi watoa huduma hospitali ya rufaa kanda ya Mbeya kwa kuwa na vifaa itatuongozea weledi wa ufanyaji kazi ili tuweze kuwahudumia vizuri wagonjwa wetu ,mara baada ya mafunzo haya kwasababu tulishapata elimu ya kutosha jinsi ya kutumia vifaa hivyo tutatoa huduma stahiki “amesema Makulila.