May 27, 2022

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Wanawake watakiwa kuendelea kukataa ukatili wa kijinsia

Na Mwandishi wetu,timesmajira,Online

WITO umetolewa kwa wanawake nchini  kuendelea kuchukua jukumu la kuongelea na kukataa vitendo vya ukatili wa kijinsia unaofanywa dhidi ya wanawake na Watoto.

Pia wametakiwa kuunganisha nguvu zao  kwa pamoja katika kulishughulikia zaidi suala hilo katika ngazi zote ikiwemo ngazi ya familia.

Akizungumza hayo jana,Jijini Dar es Salaam katika ufunguzi wa semina ya mafunzo kwa wanawake ,Mkurugenzi Mtendaji wa Mfuko wa kuwasaidia Wanawake,Mary Rusimbi amesema suala la ukatili wa kijinsia ni pana na ni refu  na sio ukatili uwe wa kupigwa tu kwa wanawake.

“Mara nyingi watu wanajua  ukatili ni ule wa kupigwa tu kwa wanawake,lakini ukiangalia linamapana marefu,leo naona watu wa Tapo la tabata  wameungana na  kuangalia kwa mapana yake suala la ukatili wa kijinsia katika kipindi hiki cha siku 16 za kupiga ukatili huo,” amesema.

“Nimefurahi sana kukutana na wakiamama wa tabata najua  watatoka na mikakati ambayo watafanyia kazi kwa ngazi ya jamii,”amesema

Mkurugenzi Mtendaji wa Mfuko wa kuwasaidia Wanawake,Mary Rusimbi akisalimiana na viongozi wa serikali za mitaa

Kwa Upande wake Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake ya Tapo Tanzania ambaye pia ni Mkurugenzi  Mtendaji wa Tabata Women Tapo,Stella Mbaga alisem taasisi yao imeamua kuwaunganisha wanawake wa tabata kwa lengo la kuwaelimisha juu ya masuala ya ukatili wa kijinsia.

Amesema  mkutano huo ni muendelezo  wa mikutano wanayofanya katika Tapo yao ya kuwakutanisha wanawake na kuwafundisha vitu mbalimbali ikiwemo masuala ya kiuchumi na kijamii.

“Siku kama hizi uwa tunajumuika na wamama na kuadhimisha siku 16 ya ukatili wa kijinsia na maadhimisho hayo yameenda sambamba na siku ya ukimwi duniani ambapo wapo wamama waliofanyiwa ukatili wa kijinsia na kusababishiwa maambukizi hayo ya ukimwi,”amesema.

Naye Mwenyekiti wa Mtaa wa Msimbazi,Godfrey Kizigo amesema taasisi hiyo,imekuwa msaada mkubwa kwa mtaa wake katika kusaidia wanawake kujitambua na kuwa vinara wa kufundisha watu wengine juu ya masuala ya ukatili.