April 25, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Polisi waua majambazi 3 wakamata silaha ya kivita na mirungi

Na Ashura Jumapili,Kagera,

JESHI la polisi Mkoani Kagera limefanikiwa kuzuia tukio la unyang’anyi wa kutumia silaha kwa kuwaua majambazi watatu ambao walipanga kufanya utekaji wa magari na kupora Mali za watu katika maeneo ya Kijiji cha Nyabugombe Kata Nyakahura Wilayani Biharamulo Mkoani humo.

Kamanda wa polisi Mkoa wa Kagera Jumaa Awadhi,alithibitisha kutokea kwa tukio wakati akiongea na waandishi wa habari ofisini kwake kuwa tukio hilo lilitokea Jana ( leo ) Desemba Mosi Majira ya saa nane usikunkatikabMilima ya Nyabugombe Wilayani Biharamulo Askari polisi walirushiana risasi na majambazi Wapato Saba na kufanikiwa kuwauwa watatu na kupata bunduki ya kivita moja aina ya AK 47 na risasi 51.

Awadhi, alisema Octoba 30 mwaka huu Majira ya saa tatu usiku jeshi la polisi Mkoani humo lilipata taarifa kutoka kwa Msiri kuwa una watu Wapato Saba wanaodhaniwa kuwa majambazi wameonekana katika Molina ya Nyabugombe wakiwa wamevalia makoti marefu na kuhisia kuwa wameficha silaha kwenye makoti hayo.

Alisema baada ya kupata taarifa hiyo Askari wa kikosi cha kupambana na ujambazi (ANT-ROBBERY) walikwenda katika maeneo hayo kufanya ufuatiliaji ( Doria ) na Majira ya saa nane usiku waliwaona watu hao na kuwasimamisha kwa lengo la kuwahoji na ili wajitambulishe wao ni akina nani ndipo walipoanza kuwashambulia Askari kwa risasi.

Alisema Askari walijibu mapigo na katika majibizano ya risasi walifanikiwa kujeruhiwa majambazi watatu kwa risasi na wengine wanne walifanikiwa kitoroka kabla hawajakamatwa.

Alisema walifanya upekuzi eneo la tukio na kufanikiwa kukuta silaha moja ya kivita aina ya AK 47 ilitofutika namba za usajili na magazine 2 zikiwa na risasi 51 na kitambulisho kimoja cha Burundi chenye jina la COYITUNGIYE VENANCIE Mkulima wa Muyinga nchini Burundi.

Alisema Majambazi hao waliojeruhiwa walichukuliwa na kufikishwa hospitali teule ya Wilaya Biharamulo na warifariki wakati wakiendelea kupatiwa matibabu.

Alisema miili ya marehemu imehifadhiwa katika chumba cha kuhifadhia maiti hospital teule ya Biharamulo kwa uchunguzi wa madaktari.

Alisema msako MKALI bado unaendelea ili kuwabaini na kuwakamata waliotoroka kabla hawajakamatwa.

Wakati huohuo alisema wanamshikilia Buruhan Juma fundi gereji miaka (38 ) mkazi wa Mtaa wa forodhani Kata ya Bakoba Manispaa ya Bukoba kwa kukutwa na kg 10 za madawa ya kulevya aina ya mirungi.

Alisema baada ya kupata taarifa za fundi huyo kufanya biashara ya dawa hizo za kulevya walifika nyumbani kwake kumpekuwa Majira ya saa 11:30 jioni na kufanikiwa kukuta mirungi gomba 142 sawa na kg 10 na pipa moja pamoja na mtambo wa kuvuta mafuta kwenye magari.

Alisema mtuhumiwa atafikishwa mahakamani baada ya upelelezi kukamilika.