May 18, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Wananchi Ngorongo rufiji wavurugana na diwani wao

Na David John Rufiji

WANANCHI wa kijiji Cha Ngorongo kata ya Ngorongo Wilayani Rufiji Mkoani pwani wameulalamikia uongozi wa kata hiyo chini ya Diwani Hassan Mpange kuhamisha ujenzi wa kituo cha Afya kilichokuwa kijengwe kijijini hapo.

Wamesema viongozi hao wamefanya maamuzi hayo kwa matakwa yao na si kwa makubaliano na wananchi na kwamba ujenzi huo wanaupeleka Kilimani hali ambayo inawachanganya wananchi wa kata hiyo.

Wakizungumza kijijini hapo mbele ya waandishi wa habari kupitia mkutano wa dharula ulioitishwa na wananchi hao. wamesema awali walikubaliana kituo hicho kijengwe katika kijiji cha Ngorongo na tayari kilikuwa kimeshaanza kujengwa kwa nguvu za wananchi na Serikali akiwemo Mbunge wa jimbo hilo Mohamed Mchengerwa ambaye alichangia Fedha na mifuko ya Saruji .

Mwenyekiti wa kijiji hicho Rajabu Ally akizungumzia sakata hilo amesema Baada ya kuingizwa pesa za ujenzi wa kituo hicho Diwani amekuwa na kauli zisizo waridhisha wananchi wake na kuamua kuachana na Kituo cha awali na kuanza mchakato wa kufyeka msitu mwingine ili kijengwe kituo cha Afya kingine kinyume na makubaliano yaliyokuwa yamefikiwa.

“Jambo hili limechanganya wananchi na ndio maana umeona mkutano huu wa dharula .wananchi hawakubaliani na hiki kunachofanyika na viongozi ngazi ya kata.”amesema Mwenyekiti Ally

Kwaupande wake Sud Mohamed amesema ili kupata ufumbuzi wa jambo hilo wanamuomba rais Samia Hassan Suluhu amemuomba Kuitupia Macho kata ya Ngorongo haswa Diwani wao ambae wamedai kuwa ni kikwazo kwa maendeleo ya kata Yao.

Ameongeza kuwa hawakubaliani na hatua ambayo diwani aneichukua ya kuhamisha ujenzi wa kituo hicho cha afya nakwamba wananchi wametumia nguvu nyingi kuhakikisha eneo hilo linajengwa Zahanati.

Naye Diwani Mpange anayelalamikiwa akizungumzia malalamiko hayo ya wananchi wa kijiji cha Ngorongo amesema yeye kama diwani hana uwezo wa kubatilisha au kuhamisha ujenzi wa kituo hicho lakini hatua hiyo imefikiwa kupitia bazara la ODC ambalo linashirikisha wenyeviti wote wa serikali za mitaa.

Amesema Kuwa walikubaliana kwa pamoja tena baada ya kujiridhisha kwamba eneo ambalo linakwenda kujengwa kituo cha afya ni rafiki na limezingatia uwiano wa vijiji vyote vinne vilivyopo ndani ya kata ya Ngorongo.

“ndugu mwandishi nimekupa ushirikiano wote juu ya uwepo wa malalamiko hayo lakini kama nilivyosema haya nimakubaliano kupitia baraza la ODC lakini pia watalaamu kutoka wilayani nao walishauri “amesema Mpange

Pia ameongeza Kuwa kuhusu Zahati inayojengwa kwenye kijiji cha Ngorongo licha zahanati hiyo kujengwa kwenye eneo si rafiki yeye kama diwani kwa kushirikiana na Mbunge wao mchengerwa wamehaidi kutoa mifuko ya saruji 100 nahuku akishauri Zahanati hiyo isogezwe kwenye eneo lafiki kwasababu ilipo sasa panajaa maji.