May 18, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Watumiaji wa bangi na mirungi wasakwa

Iddy Lugendo, Timesmajira online

MAMLAKA ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya nchini (DCEA) imesema kuwa, kila Mtanzania ana wajibu wa kutoa taarifa yoyote inayohusiana na uhalifu wa dawa za kulevya hapa nchini.

“Mamlaka tunafanya kazi kutokana na jamii, Kwa niaba ya Kamishina Jenerali wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya nchini, Gerald Kusaya niwahakikishie kuwa, mtu au watu ambao wataleta taarifa zao katika mamlaka zinazohusiana na uhalifu wa dawa za kulevya, tutazipokea kwa uaminifu wa hali ya juu na tutamtunzia siri, hivyo msiwe na hofu yoyote kama mna taarifa”

Aidha Kamishna Msaidizi Kinga na Huduma za Jamii Moza Makumbuli amebainisha kuwa, dawa za kulevya ambazo ni tatizo kubwa hapa nchini ni pamoja na bangi na mirungi.

Kwa mujibu wa Sheria Namba 5 ya Mwaka 2015, kilimo na biashara ya bangi katika Taifa letu ni haramu , hivyo kujihusisha kwa namna yoyote na bangi kwa maana ya kulima, kuuza, kuhifadhi, kutumia au kwa namna nyingine ni kosa la jinai.