April 25, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Kaimu Mhariri mkuu wa Jarida la Afya ya jamii Tanzania (TPHB) Dkt. Julius Massaga.

Waandishi wajengewa uwezo kuripoti habari sahihi za afya

Na Mwandishi Wetu

IMEELEZWA kuwa hofu miongoni mwa wananchi katika jamii kipindi yanapotokea magonjwa ya milipuko husababishwa na upotoshwaji wa taarifa ambazo nyingi zinakuwa si za kweli kutokana na ujio wa teknolojia.

Akizungumza na kwenye mafunzo ya kuwajengea uwezo waandishi wa habari yaliyofanyika kwa siku mbili Jijini Dar es Salaam,Kaimu Mhariri Mkuu wa Jarida la Afya ya Jamii Tanzania (TPHB) Dkt.Julius Massaga alisema kuwa kumekuwa na mtindo wa matumizi mabaya ya mitandao kwa utoaji taarifa zisizo mbalimbali ambazo si sahihi na kusababisha taaruki.

Kaimu Mhariri mkuu wa Jarida la Afya ya jamii Tanzania (TPHB) Dkt. Julius Massaga akitoa somo kwa waandishi wa habari kuhusiana na namna ya kuripoti habari za afya.

“Kuna baadhi ya watu walihusika katika utoaji wa taarifa kuhusiana na Corona ambazo si kweli na hii ilichangia kuongeza hofu kwa wananchi na haya ndio matumizi mabaya ya teknolojia,’ alisema.

Alisema kuwa ni vyema waandishi wa habari za afya wakaripoti taarifa kwa kuzingatia maadili ya taaluma yao kwa kufuata sheria jambo ambalo litasaidia kutoa majibu kuhusu masuala mbalimbali katika sekta ya afya pamoja na kuepuka habari ambayo inaweza kujenga hofu katika jamii.

Naye Mkuu wa Mawasiliano kutoka Wizara ya Afya Gerald Chami,alisema kuwa lengo la kutoa semina kwa waandishi wa habari ni kuwajengea uwezo ambao utawasaidia kuripoti taarifa za afya kutoka vyanzo vya habari vilivyokuwa sahihi.

Mkuu wa Mawasiliano kutoka Wizara ya Afya Gerald Chami

“Tumetoa semina kwa wanahabari kwa siku mbili ili kuwasaidia waripoti habari za kweli na kuepuka kutoa taarifa ambazo zinaweza kuleta hofu kwa wananchi” alisema Chami.

Akifunga mafunzo hayo Kaimu Mkurugenzi wa Uratibu na Ukuzaji Tafiti kutoka Taasisi ya utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR) Dkt.Mary Mayige,alisema kuwa mafunzo hayo maalumu kwa wanahabari yanakwenda kuwajengea uwezo katika kuripoti habari za afya.

Dkt.Mayinge alisema kuwa wapo tayari wakati wowote kutoa taarifa na ufafanuzi kwa waandishi wa habari ili kuhakikisha wapata taarifa sahihi.

Hata hvyo ameawata waandishi wa habari kuyafanyia kazi kwa vitendo yale ambayo wamefundisha ili kuleta matokeo chanya katika jamii.

Semina hiyo imeandaliwa na Tanzania Public Health Bulletin (TPHB) kwa kushirikiana na Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kwa kutoa mafunzo maalumu kuhusiana na namna bora ya kuripoti habari za afya ambapo kupitia mradi wa Takwimu na Sera za afya kwa kushirikiana na wadau wa maendeleo, Wizara ya afya, Taasisi ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR) na ofisi ya mganga mkuu wa Serikali.

Uwepo wa jarida la afya nchini wamerahisisha namna ya kupata taarifa muhimu za afya kupitia jarida hilo ambalo hutoka kila baada ya miezi mitatu na lililosheheni taarifa na matokeo ya tafiti mbalimbali za kisayansi.