April 24, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Visababishi saratani shingo ya kizazi

SARATANI ya shingo ya kizazi ni aina ya saratani inayotokea katika chembechembe za shingo ya kizazi, ambayo ni sehemu ya chini ya mji wa mimba (uteri) inayoungana na uke.

Aina mbalimbali za virusi aina ya papilloma wamethibitishwa kusababisha saratani hii ambayo hujitokeza kwa wingi miongoni mwa wanawake duniani kote,hususani wenye umri kati ya miaka 20 na 39.

Saratani ya shingo ya kizazi ni ya pili miongoni mwa saratani zinazowapata wanawake ambapo wagonjwa wapya wapatao 529,828 hugunduliwa kila mwaka, asilimia 85 wakiwa ni katika nchi zinazoendelea.

Inabakia kuwa ya pili baada ya saratani ya matiti kwa kusababisha vifo vitokanavyo na saratani, ambapo huchangia asilimia 10 ya vifo vitokanavyo na saratani mbalimbali kwa wanawake. Inakadiriwa kuwa zaidi ya wanawake 275,000 hufa kila mwaka kwa ugonjwa huu, idadi kubwa ni kutoka nchi zinazoendelea ikiwemo Tanzania.

AINA ZA SARATANI YA SHINGO YA KIZAZI

Kuna aina mbili za seli kwenye shingo ya kizazi (cervix) ambazo ni squamous cell na glandular calls, hivo saratani ambayo huanzia kwenye seli za squamous huitwa “squamous cell carcinoma” na saratani inayoanzia kwenye seli za glandular huitwa “adenocarcinoma”.

Jambo muhimu la kufahamu ni kwamba Saratani inapoanza huwa ni vigumu sana kuigundua kwani haioneshi dalili zozote, hivo unaweza usigundue mpaka pale saratani imefikia hatua mbaya Zaidi, pale ambapo dalili kama kutokwa na majimaji au maumivu wakati wa tendo la ndoa.

Seli za kansa ya shingo ya kizazi hukua taratibu na huchukua miaka michache kwa seli za kawaida kubadilika kuwa seli za kansa, ndio maana inashauriwa kufanya vipimo mara kwa mara ili kugundua mapema.

VISABABISHI

Wanawake wengi wanaopata ugonjwa huu huwa na kisababishi kimoja au zaidi kinachojulikana ambacho huongeza hatari ya kuupata,visababishi vikuu ni kuanza vitendo vya ngono katika umri mdogo (chini ya miaka 16),kuwa na mahusiano ya kimwili na zaidi ya mwanaume mmoja,maambukizo ya virusi vya HPV (Human papilloma virus).

Pia maambukizo ya magonjwa ya zinaa,umri zaidi ya miaka 30,upungufu wa kinga mwilini (VVU/UKIMWI),uvutaji wa sigara,kupata mimba katika umri mdogo
idadi kubwa ya watoto na kuzaa mara kwa mara,hali duni ya kiuchumi,kuwa na mahusiano ya kimwili na mwanaume ambaye mkewe alikufa kwa saratani ya shingo ya kizazi.

Visababishi vingine ni kuwa na mahusiano ya kimwili na mwanaume ambaye hajatahiriwa,historia ya saratani ya shingo ya kizazi katika familia,kuanza vitendo vya ngono katika umri mdogo na kuwa na mahusiano ya kimwili na zaidi ya mwanaume mmoja ni visababishi vinavyoongoza.

Pia maambukizo ya virusi vya HPV (Human papilloma virus), huchangia kwa kiasi kikubwa katika kusababisha ugonjwa huu.

DALILI SARATANI YA SHINGO YA KIZAZI

Katika hatua za awali za ugonjwa huu kunaweza kusiwe na dalili zozote. Lakini, kadri muda unavyosonga dalili bayana za awali hujitokeza kama kutokwa na damu ukeni kusiko kawaida mfululizo,kutokwa na damu ukeni baada ya tendo la ndoa.

Dalili nyingine ya saratani ni kupata maumivu makali ya tumbo na nyonga,
maumivu wakati wa tendo la ndoa,kutokwa na majimaji ukeni kusiko kawaida yenye harufu na maumivu ya tumbo chini ya kitovu.Muda unavyosonga zaidi, ugonjwa huu unaweza kusambaa kwenda tumboni, mapafuni au popote pale mwilini.

Dalili nyinginezo ni kama maumivu ya mgongo, maumivu ya nyonga, miguu kuuma na/au kuvimba, uchovu, kukosa hamu ya kula, kupungua uzito, kutokwa na damu kwa wingi ukeni, kutokwa na mkojo au kinyesi ukeni (fistula) na kuvunjika mifupa kwa urahisi.

WATU GANI WAPO KWENYE HATARI KUBWA YA KUPATA

Kuna sababu zilizo ndani ya uwezo wako ambazo unaweza kuzifanyia kazi na kuunguza hatari ya kupata saratani hii, japo pia kuna njia ambazo ni vigumu kuepuka za ziko nje ya uwezo wetu kama vile uwepo wa saratani hii katika historia ya familia yako mfano kama mama ama dada yako aliwahi kupata saratani hii basi unaweza kuwa kwnye hatari kubwa nawe kupata.

Makundi mengine ni kama wanawake kwenye umri kati ya miaka 20-50 wapo kwenye hatari zaidi matumizi ya vidonge vya kupanga uzazi kwa muda mrefu.

Kuzorota kwa kinga ya mwili husabisha kuongezeka kwa athari ya virusi wa HPV wanaoletekeza kansa ya shingo ya kizazi.Wanaopata ujauzito katika umri mdogo chini ya miaka 17 wapo kwenye hatari Zzidi ya kupata saratani hii.

MATIBABU YA SARATANI YA SHINGO YA KIZAZI

Tiba ya saratani ya shingo ya kizazi hutegemea na hatua ya ugonjwa husika, na inahusisha kufanyiwa upasuaji na kuondoa mfuko wa mimba (uterus) na viungo vingine kama ovari na mirija ya uzazi

Matibabu kwa kutumia dawa kali(chemotherapy) ili kuongeza muda wa kuishi
matibabu kwa njia ya mionzi ili kuua seli za saratani.kufanyiwa uchunguzi wa kitabibu mara kwa mara.

Kupata chanjo dhidi ya virusi vya HPV kabla ya kuanza vitendo vya ngono.
kupata elimu sahihi kuhusu ugonjwa huu.Kujiepusha na mambo hatarishi yanayosababisha kuupata ugonjwa huu.Ugunduzi wa mapema katika hatua za awali za ugonjwa huu na kupatiwa matibabu stahiki na kwa wakati.

MAMBO 10 UNAYOWEZA KUFANYA KUPUNGUZA HATARI YA KUUGUA

Usivute sigara wala kutumia tumbaku ya aina yoyote,hakikisha nyumbani kwako hamna moshi,kula chakula chenye afya,kunyonyesha kunapunguza hatari kwa mama kuugua saratani,hakikisha watoto wako wanapata chanjo dhidi ya hepatatis B na HPV,punguza uchafuzi wa hewa ndani na nje ya nyumba

Pia jishughulishe kuupa mwili mazoezi,punguza unywaji wa pombe,jitahidi kufanyiwa ukaguzi wa mapema kutambua uwepo wa saratani.

Shirika la Afya Duniani (WHO) limeeleza kuwa saratani ya shingo ya kizazi inaua zaidi ya wanawake 300,000 kila mwaka duniani, wengi kutoka nchi zinazoendelea. J

WHO inaeleza kuwa saratani ya shingo ya kizazi ambayo ikigundilika mapema inatibika, husababishwa na kirusi cha Human Pappiloma Virus na huambukizwa kwa njia ya kujamiiana.

Princess Nothemba Simelela ambaye ni mkurugenzi mkuu msaidizi wa WHO anasema kuwa tatizo lililopo katika nchi zinazoendelea ni ukosefu wa wataalamu wenye ujuzi wa kuwapima wanawake na kuwatambua kama wana saratani ya shingo ya kizazi.

Mkurugenzi wa Kinga na Daktari bingwa magonjwa ya saratani wa Taasisi ya magonjwa ya Saratani ya Ocean Road (ORCI),Dkt.Crispin Kahesa anasema asilimia kubwa ya wagonjwa wanaofika katika hospitali hiyo wanakuwa tayari wamefika katika hatua za mwishoni.

Anasema wagonjwa wamekuwa wakidanganywa juu ya dawa za saratani hivyo wengine kuacha kuja hospitali na kwenda kwa waganga wa kienyeji hadi wanapofika hatua za mwisho.

Pia Dkt.Kahesa anasema kwa sasa hali ya magonjwa ya saratani yamekuwa yanaongezeka na kubadilika kutoka katika virusi na kuwa saratani inayotokana na mfumo wa ulaji chakula .

Dkt.Kahesa amewataka Watanzania kujitokeza kwa wingi katika hospitali yao kufanya uchunguzi wa saratani bila malipo yeyote.

Kwa Upande wake Kaimu Mkurugenzi wa Tiba wa Taasisi hiyo,Dkt.Mark Mseti anasema saratani ni kundi la magonjwa yasioambukiza .

Anasema saratani zinazoongoza katika taasisi hiyo ni pamoja na saratani ya Shingo ya Kizazi,Matiti,Ngozi ya Kapoji Sarcoma,Koo la Chakula na Saratani ya kichwa na Shingo.

Anasema kuwa tiba ya mionzi kwa sasa inatolewa katika hospitali zote za Kanda zikiwemo Hospitali ya Rufaa ya Mbeya, Benjamin Mkapa ya Dodoma, Bugando Mwanza, KCMC Kilimanjaro na Ocean Road Yenyewe ambayo inatoa tiba ya miozni na matibabu mengine ya kibingwa kwa magonjwa ya Saratani.

Mkurugenzi wa Kinga na Daktari bingwa magonjwa ya saratani wa Taasisi ya magonjwa ya Saratani ya Ocean Road (ORCI),Dkt. Crispin Kahesa anasema asilimia kubwa ya wagonjwa wanaofika katika hospitali hiyo wanakuwa tayari wamefika katika hatua za mwishoni.

Amesema wagonjwa wamekuwa wakidanganywa juu ya dawa za saratani hivyo wengine kuacha kuja hospitali na kwenda kwa waganga wa kienyeji hadi wanapofika hatua za mwisho.

Anasema kwa sasa hali ya magonjwa ya saratani yamekuwa yanaongezeka na kubadilika kutoka katika virusi na kuwa saratani inayotokana na mfumo wa ulaji chakula .

Dk.Kahesa amewataka Watanzania kujitokeza kwa wingi katika hospitali yao kufanya uchunguzi wa saratani bila malipo yeyote.

Mkurugenzi wa Tiba wa Taasisi hiyo,Dkt.Mark Mseti anasema saratani ni kundi la magonjwa yasioambukiza, Anasema kuwa saratani zinazoongoza katika taasisi hiyo ni pamoja na saratani ya Shingo ya Kizazi,Matiti,Ngozi ya Kapoji Sarcoma,Koo la Chakula na Saratani ya kichwa na Shingo.