May 18, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Mkurugenzi wa kampuni ya Ng’ara Craft inayojihusisha na masuala ya ubunifu na utengenezaji wa Mishumaa, Anastazia Nnungu akiongea na baadhi ya wanawake na vijana walihudhuria mafunzo ya kutengeneza mishumaa.

Vijana watakiwa kujikita katika ujasiriamali

Na Penina Malundo,TimesMajira,Online

WITO umetolewa   kwa vijana nchini kuhakikisha wanajikita katika ujasiriamali ambao kwa kiasi kikubwa utaweza kuwaongezea  kipato cha kujikimu kimaisha.

Mkurugenzi wa kampuni ya  Ng’ara Craft inayojihusisha na masuala ya ubunifu  na utengenezaji wa Mishumaa, Anastazia Nnungu amesema  ujasiriamali unaweza kuwa rahisi endapo mtu akiamua kujituma katika kitu anachotaka kukufanya na kuhakikisha anakitafutia soko.

Amesema kampuni yao inafanya utengenezaji  wa mishumaa ya nta ya nyuki (beeswax candles) ambapo lengo la utumiaji wa nta katika utengenezaji wa mishumaa ni kutokana na faida zake kwenye mazingira. 

“Beeswax ni natural air purifier ambayo inasaidia kunyonya sumu, vumbi na molds kwenye hewa na  inapunguza sana aleji au ugonjwa wa pumu kutokana na ile harufu yake,”amesema na kuongeza 

“Wazo la kufanya hivi lilikuja baada ya kupata changamoto ya utumiaji wa mishumaa mingine kuleta shida kwa watoto wangu hivyo nikaamua kufanya utafiti wa utumiaji wa nta ya nyuki ambapo mishumaa mingine utumia malighafi ya Mafuta ya Petroleum,”amesema Aidha Nnungu amesema katika kuongeza thamani bidhaa zao wameamua kufanya utafiti wa baadhi ya malighafi ambazo zinasaidia kufukuza Mbu na kuchanganya katika uzalishaji wa bidhaa zao.