May 5, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Utafiti:Unene kupita kiasi janga jipya maeneo ya mijini

Na Aveline Kitomary,TimesMajira Online,Dar es Salaam.

UTAFITI uliofanywa na Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete(JKCI) umebaini kuwa uzito mkubwa umekuwa janga la kiafya kwa watu wanaoishi maeneo ya mijini.

Utafiti huo ulifanyoka katika jiji la Dar es Salaam ulihusisha jumla ya washiriki 6691 waliojiandikisha ambapo umri wa watu hao wa wastani ulikuwa miaka 43.1 na wanaume walikuwa asilimia 54.2 ya washiriki wote.

Dkt.Pedro Pallangyo ambaye ni mshiriki wa utafiti huo aliiambia Jarida la Majira ya Afya kuwa matokeo ya utafiti yalionesha kuwa uzito mkubwa ni tatizo ambapo kati ya watu 6691 waliofanyiwa utafiti huo asilimia 67.2 walikuwa na uzito mkubwa huku wakipata madhara.

“Katika utafiti huo pia tuliangalia vitu vinavyohusiana na uzito huo na pia madhara wanayoweza kupata watu wenye uzito mkubwa ikiwa ni hatari ya kupata ugonjwa wa kisukari na shinikizo la damu.

“Tulibaini kuwa mabadiliko ya magonjwa na idadi ya watu yanasababishwa
mabadiliko ya lishe kwa watu ikihusisha vyakula na vinywaji wanayotumia,watu wamekuwa hawajali kula vyakula vya asili badala yake huzingati vile visivyo vya asili na wanakunywa vinywaji vyenye sukari zaidi kama soda,juisi na zingine bila kuzingatia unywaji mkubwa wa maji,”anabainisha Dkt.Pallangyo.

Utafiti huo pia ulianisha kuwa kwa zaidi ya miongo mitatu viwango vya uzito kupita kiasi na unene vimekuwa karibu mara tatu hadi sasa kuathiri zaidi ya theluthi ya idadi ya watu ulimwenguni.

Pamoja na hayo kila wakati upo mzigo wa lishe duni,Kusini mwa Jangwa la Sahara (SSA) inashuhudia ongezeko kubwa ya unene kupita kiasi.

“Tulilenga kuchunguza kuenea na sababu zinazohusiana na unene kupita kiasi kati ya wakazi wa jiji la Dar es Salaam nchini Tanzania,Washiriki wa utafiti huu waliajiriwa wakati wa uchunguzi wa jamii uliofanywa.

“Takwimu za kijamii na kliniki zilikusanywa kwa kutumia muundo wa dodoso wakati wa uandikishaji tuliangalia tabia za lishe, vipimo vya ‘anthropometric’ na shinikizo la damu.

“Uchambuzi wote wa takwimu umetumia programu ya STATA v11.0,mraba wa Pearson Chi na Jaribio la Wanafunzi lilitumiwa kulinganisha anuwai ya makundi na endelevu,”Ulibainisha utafiti huo.

Dkt.Pallangyo ambaye pia ni Daktari Bingwa wa Moyo anasema Zaidi ya theluthi mbili ya washiriki walikuwa watumiaji wa pombe na aslimia 6.9 walikuwa na historia nzuri ya kuvuta sigara.

“Asilimia 88 ya asilimia tatu ya washiriki walikuwa hawanyi kazi,asilimia 4.7 walikuwa na historia ya ugonjwa wa kisukari na asilimia 18.1 walijulikana kuwa wana shinikizo la damu.

“Uzito wa kupita kiasi na unene kupita kiasi ulionekana katika asilimia 34.8 na asilimia 32.4 ya washiriki,Kati ya washiriki wenye uzito kupita kiasi na wanene kupita kiasi,asilimia 32.8 walikuwa na maoni potofu ya kuwa na uzito wa afya.

“Katika Umri wa miaka 40 kwa wanawake walikuwa hawatumii kifungua kinywa (break fast) na pia kwa kiasi walikuwa hawajishughulishi,unywaji wa maji mdogo,matumizi ya vinywaji baridi, ulaji wa chakula haraka haraka, mboga mboga na matunda.

“Unywaji wa pombe ulikuwa wa kiwango kikubwa na uvutaji sigara kidogo,”anaeleza.

Dkt.Pallagyo anasema hatua za haraka zinahitaji za kuweka sera kwa maeneo ya mijini ikiwa ni pamoja na mtindo bora wa maisha kama mfumo wa ulaji na shughuli za mwili.

“Sehemu kubwa ya washiriki walikuwa wanene kupita kiasi,viwango vya kutokuwa na shughuli za mwili na kula kiafya ni ya juu sana.

“Kwa kuzingatia hii,mikakati ya kijamii na anuwai ya afya ya umma kukuza na kudumisha afya ikiwemo kula na shughuli za mwili zinahitaji hatua ya haraka katika mji wa mijini wa Tanzania.

“Mapendekezo yetu ni lazima kufanyika kitu cha kuzuia magonjwa yasiyo ya kuambukiza ,Wizara itengeneza sera ya jamii kuzingatia mtindo bora wa maisha kwa watu,”anashauri Dkt.Pallangyo.