May 8, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

UTAFITI: Chloroquine haiwezi kutibu Corona

Na Mwandishi Wetu

WASHINGTON, Ripoti ya utafiti iliyochapishwa katika jarida la New England Journal of Medicine ambayo ni matokeo ya wanasayansi walioongozwa na kikosi kazi kutoka Chuo Kikuu cha Columbia umebainisha kuwa, watu walioathiriwa na virusi vya corona (COVID-19) ambao wanatumia hydroxychloroquine (Chloroquine) kama dawa
maendeleo yao kiafya si ya kuridhisha kama wale ambao hawatumii kabisa.

Matokeo ya utafiti huo yalichapishwa mapema wiki hii ikiwa ni moja wapo ya hatua kubwa ya utafiti dhidi ya ya dawa hiyo, dawa ambayo iliidhinishwa na Mamlaka ya Chakula ya Marekani kutibu malaria na magonjwa mengine ikiwemo COVID-19.

Dkt.Neil Schluger ambaye ni Mkuu wa Kitengo cha Magonjwa ya Mapafu, Mzio na Dawa Muhimu kutoka Columbia na timu yake walichunguza zaidi ya wagonjwa 1,300 ambao wamelazwa katika Hospitali ya New York-Presbyterian ya Chuo Kikuu cha Columbia Kituo cha Irving ambacho ni maalum kwa wagonjwa wa COVID-19.

Kwa mujibu wa ripoti hiyo miongoni mwa wagonjwa hao walipewa hydroxychloroquine kwa muongozo maalum, ambao uliwawezesha madaktari kuweza kutambua aina ya dawa ambayo imeidhinishwa kwa ajili ya kukabiliana na visa vya COVID-19 katika kipindi hiki cha utafiti na hakuna matokeo chanya.

Asilimia 60 ya wagonjwa waliopewa hydroxychloroquine kwa siku tano, hawakuonyesha mabadiliko yoyote katika upumuaji, hali ilikuwa mbaya ikilinganishwa na watu wasipopata dawa hiyo hii ikiwa ni kwa mujibu wa utafiti huo.

TAARIFA KAMILI ITAKUWEPO KWENYE GAZETI LA MAJIRA…