Na David John
MkUU wa ujumbe wa Umoja wa Ulaya Manfreo Fanti akiwa pamoja na mabalozi wa Nchi wanachama wa Eu Nabil Hajlaoui ambaye ni balozi wa ufaransa nchini na wengine wamekutana na waandishi wa habari na kuzungumzia siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia.
Akizungumza katika mkutano huo mbele ya vyombo vya habari uliofanyika katika kituo cha utamaduni cha ufaransa Fanti alisema wamefanya mkutano huo kuwasilisha mpango wa mwaka huu kuhusu siku 16 za kupinga Ukatili wa Kijinsia nchini Tanzania.
Amesema kuwa siku 16 za Kupinga Ukatili wa Kijinsia ni kampeni ya kimataifa inayolenga kuongeza uelewa kuhusu athari za ukatili, hasa kwa wanawake na wasichana wadogo.
“kampeni hii inasisitiza kwamba unyanyasaji dhidi ya wanawake, kwa namna yoyote, ni ukiukwaji wa
haki za binadamu na Kwamba wanawake wote, wasichana, wanaume na wavulana katika utofauti wao wote – wanapaswa kuchukua msimamo dhidi yake.
Nakuongeza “Hapa ni Nchi Wanachama wa EU zimeungana na UNFPA na washirika wamejitolea kukomesha unyanyasaji wa kijinsia.
Amesema Katika siku 16 za mwaka huu za uharakati balozi za Ubelgiji, Denmark, Finland, Ufaransa, Ujerumani, Ireland,
Uholanzi, Uhispania, Uswidi na Ujumbe wa EU pamoja na wadau wa kitaifa na UNFPA watapanga matukio kadhaa ya umma jijini Dar es Salaam na mkoa wake kuanzia Novemba 25 hadi Desemba 10 ,2021.
Fanti ameongeza kuwa Maadhimisho hayo yatahitimishwa kwa tuzo ya Bingwa wa Pamoja wa UWAKI na tamasha la kukusanya fedha kuandaliwa.na timu ya Ulaya, Muungano wa MKUKI, WiLDAF pamoja na UNFPA.
Amefafanua kuwa tukio hilo litafanyika Jumatano Desemba 8,2021, kuanzia saa 19:00 Jioni katika Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam na maonyesho ya watu mashuhuri wa kitaifa Akiwamo Ben Pol, Nandy, Siti na Bendi, Muziki wa Bedja na Shikandol .
Naye Balozi wa ufaransa Hajlaoui akizungumzia siku 16 kupinga ukatili wa kijinsia hususani Tanzania amesema ni muhimu kuendelea kuwainua wanakwake na kuondoa mfumo dume ili kuwa sawa na ameshauri nivema kuepukana na hilo ili kuleta usawa.
Hajlouoi ameongeza kuwa lazima elimu iendelee kutolewa hata kwa kupitia siasa na bahati nzuri Tanzania inaongozwa na rais mwanamke na kwamba kwa ufaransa ukatili wa kijinsia upo kwenye upande wa elimu lakini wanajalibu kutafuta ufumbuzi na wanapiga hatua kubwa.
More Stories
Kapinga atoa maagizo TANESCO ,kuhusu Vijiji vinavyolipia gharama ya mijini kuunganisha umeme
Ukiukaji wa Uhuru wa Kidini na Kutovumiliana Huzusha Malumbano ya Kimataifa
NLD kipo tayari kwa uchaguzi wa Serikali za Mitaa