Na Joyce Kasiki,Timesmajira online,Dodoma
KIASI cha Shilingi bilioni 250 zinatarajiwa kuzalishwa katika kipindi cha miaka mitano kupitia mkataba wa mauziano wa tani 60,000 kwa kampuni ya Kimataifa ya uchimbaji Makaa ya Mawe nchini Uswis (ABSA).
Akizungumza jijini Dodoma katika hafla ya utiaji saini mkataba wa Makaa ya Mawe ya Mkoa ya Songwe katika Mgodi wa Kabulo kupitia kampuni ya ABSA, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Madini la Taifa (STAMICO), Dkt.Venance Mwasse amesema,mkataba huo unakwenda kuongeza mapato zaidi.
“Kwa hiyo mkataba huu ni mkubwa na ni wa kihistoria kwa nchi kwa kuwa utasaida kwenye masuala ya kiuchumi.”amesema na kuongeza kuwa
“Makaa hayo yatasafirishwa kutoka Kiwira hadi Bandari ya Mtwara na tayari magari 300 yatakayokuwa na madereva wawili kila moja yameandaliwa hivyo watakuwa 600 jumla, pia kutakuwa na nguvu kazi takribani watu 200,”
Dkt.Mwasse amesema,mkataba huo utatekelezwa kupitia vifungu walivyokubaliana na mwekezaji huyo huku akimuhakikishia kuwa yupo kwenye mikono salama na matokeo mazuri na huduma wataziona wakati wa utekelezaji wa mradi wa uchimbaji makaa hayo ya mawe.
Naibu Waziri wa Madini Dkt.Steven Kiruswa amesema Serikali kupitia shirika la STAMICO itakusanya mapato wastani wa shilingi bilioni 4.16 kwa mwezi sawa na wastani wa shilingi bilioni 50 kwa mwaka.
Mbali hilo pia Shirika litatoa ajira kwa vijana wa kitanzania zisizo za moja kwa moja 600 na fursa nyingine kupitia mradi huo.
“Ni matumaini yangu makubaliano tuliyokubaliana ABSA yataleta tija katika nchi hizo na kuishukuru STAMICO kwa maamuzi ya kukubaliana kufanya biashara nchini ambapo itasaidia kuwapatia vijana ajira.
Akizungumza katika hafla hiyo, Rais wa Kampuni ya ABSA, Gerges Schmickrath ameishukuru wizara ya Nishati kupitiaShirika lake la STAMICO kwa kuiamini kampuni yake na hatimaye kupata kibali cha kuwekeza katika mradi wa makaa ya mawe ambao amesema utakuwa na manufaa kwa watanzania na Taifa kwa ujumla.
Schmickrath amesema kutokana na Serikali kuonyesha imani kwao na wao watafanya kazi itakayoleta tija kama ilivyokusudiwa.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Drumlin Construction LTD ambaye ni msafirishaji wa makaa hayo nchini, Linus Seushy amesema kuwa wamejiandaa kuhakikisha kila kitu kinafanyika kama kilivyopangwa kwa maslahi mapana kwa Taifa.
More Stories
Kambi ya wanasheria Katavi kuwajengea uwezo wananchi
Serikali yaimarisha uchumi wa kidigitali kukuza biashara mitandaoni
RAS Tanga aipongeza Lushoto DC kuvuka lengo mapato ya ndani