May 20, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

TRAMEPRO watoa Elimu kwa Waganga wa Tiba asili

Na David John, TimesMajira Online, Pwani

KATIBU mkuu wa shirika la Dawa Asili na Ulinzi wa Mazingira TRAMEPRO Bonivetura Mwalongo amewataka Matabibu na waganga wa Tiba asili nchini kuhakikisha wanafanya kazi zao kwa kuzingatia sheria , Kanuni na taratibu zinazowaongoza kwa maslahi mapana ya sekta hiyo.

Mwalongo ameyasema hayo Mei 30 2022 mbele ya waandishi wa habari katika kikao maalumu kilichowakutanisha waganga wa tiba asili waliopo mkoa wa Pwani katika Halmashauri ya Mji wa Chalinze kijiji cha Vigwaza ambapo amesema wao kama Shirika la Dawa Asili na Ulinzi wa Mazingira kazi yao kubwa ni kutoa elimu ya ufahamu kwa waganga ili waweze kufuata utaratibu ,miongozo ambayo wanapewa na Mamlaka husika kwa maana Wizara ya Afya.

Amesema kuwa waganga wengi wanaingia kwenye changamoto kutokana na kutojua taratibu ,kanuni,sera.pamoja na sheria zinazowaongoza hivyo wao kama Shirika malengo yake tangu kuazishwa kwake nikuhakikisha wanawafikia waganga na kuwakumbusha umuhimu wa kufuata sheria ikiwa pamoja na kufanya shughuli hizowakiwa wamesajiliwa .

“Leo tupo hapa Vigwaza kama mnavyoona na huu ni muendelezo tu wa utoaji elimu ya kukumbushana na tuliaza siku kadhaa zilizopita ndani ya Halmashauri ya Mji wa Chalinze kikubwa ni kuwakumbusha tu waganga umuhimu wa kuzingatia sheria na miongozo mbalimbali inayotolewa na serikali yetu na ndio maaana hata mikutano hii inashirikisha Mamlaka zote zinazohusika.”amesema Katibu mkuu Mwalongo

Ameongeza kuwa waganga wanahaki ya kufikiwa na kupewa elimu juu ya miongozo ya kisheria na wao kama Shirika ndio wanalolifanya kama sehemu ya majukumu ya TRAMEPRO na watahakikisha wanaendelea kushirikiana na watendaji wa kata ,wenyeviti wa serikali za mitaa ,waratibu,pamoja na Jeshi la Polisi ili kuona sekta ya dawa asili inapata heshima kubwa na waganga wanaheshimika .

Akizunguzumzia uwepo Royal Tour amesema wao kama shirika walishatoa pongezi kwa Rais kwa kazi kubwa ambayo ameifanya na kimsingi kupitiasekta hiyo ya tiba asili haiwezi kubaki nyuma kwani huwezi kuzungumzia Royal Tour bila kuitaja sekta ya dawa asili ambayo kwa kiasi kikubwa inatoa huduma za kiafya kwa watu na jamii kwa ujumla.

Kwaupande wake Mwenyekiti wa serikali ya kijiji cha Vigwaza Ramadhan Komi amewataka waganga hao wa tiba asili kushirikiana kufanya kazi kwa umoja,kuwa wa wazi na wakweli pia kuwa tayari kulinda mazingira yanayowazunguka ili yasichomwe moto kulinda uoto wa asili utakao saidia upatikanaji wa dawa zitakazowasaidia wao na vizazi vya baadae.

“Lengo kuu la kukutana hapa ni kuunganisha mawazo kwasababu masuala ya afya yanahitaji mashirikiano kwani masuala haya yanahitaji ujuzi hivyo ndio sababu kubwa yakukutana hapa “Amesema Mwenyekiti wa shirikisho la vyama vya waganga wa tiba asili Pwani

Kwaupnde wake Tatu Katoto amaesema sekta ya dawa asili bado kuna changamoto kwani wagonjwa wengi wanafika kwao kabla ya kupita hospitali lakini kinachotakiwa lazima kwaza aende hospitali wakishindwa ndipo wanapoweza kuja kwao wakiwa na nyaraka walizotokanazo hospitali na kuhusu elimu waliyoipata kutokana na kikao hicho wamefurahishwa nayo kwani kupitia kikao hicho wamepta kujua mengi yanayohusu sekta hiyo ya tiba asili.

Katika kikao hicho changamoto kubwa iloiyojitokeza ni waganga kutojua mahala sahihi ambapo wanweza kupata usajili utakahalalisha shughuli wanazozifanya na badala yake wamejikuta wakitoa fedha na mwisho wa siku hawapati usajili wa kazi zao kwa wakati ama kukosa kabisa huku hela wakiwa wakiwa wameshatoa.