May 19, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

TRA wakabidhi madarasa, madawati shule ya msingi kisarawe II

Na Mwandishi wetu, Timesmajira online

MAMLAKA ya Mapato Tanzania (TRA) imekabidhi madarasa mawili pamoja na madawati 100 wa shule ya msingi Kisarawe II yenye thamani ya shilingi millioni 50.

Hatua hiyo inakuja katika kupunguza chagamoto ya madawati pamoja na vyumba vya madarasa katika shule hiyo.

Akizungumza katika hafla ya makabidhiano, Naibu Kamshina wa walipaKodi wakubwa, Eunice Luheluka amesema TRA imeamua kurudisha kidogo kwa jamii ambacho kimetokana na kile kilichokusanywa ili kuweza kufikia malengo.

“Ni kawaida kwa TRA kuwa na wiki ya shukrani kila mwaka ambapo Kwa mwaka huu tumeamua kukirudisha katika shule ya msingi kisarawe II,”amesema.

Aidha Naibu Kamshina huyo amesema anaimani vyumba hivyo vya madarasa pamoja na madawati vitatumika vizuri ili kuboresha mazingira ya shule hiyo.

“Tunatambua bado kunauhitaji katika shule hii lakini kwa kidogo hiki tulichotoa tunaamini tutaendelea pia ni ishara ya kuleta matumaini Kwa watoto wetu,”amesisitiza.

Aidha amesema TRA itaendelea kusimamia na kusaidiana na Serikali katika kukuza elimu katika maeneo mbalimbali ya nchi.

Awali Mkuu wa shule hiyo, Joseph Kavishe amesema shule hiyo inajumla ya wanafunzi 1408 kati ya hao wavulana ni 703 huku wasichana wakiwa 705 pamoja na walimu 23.

Amesema fedha walizopewa na Mamlaka ya mapato Tanzania zimeweza kujenga vyumba vya madarasa mawili pamoja na madawati 100 .

“Tulipokea kiasi cha shilingi millioni 50 kutoka Mamlaka ya mapato Tanzania TRA Desemba 2012 ambapo Februari tulianza ujenzi rasmi,”amesema.

Pia ameishukuru TRA Kwa msaada huo kwani unakwenda kuwawezesha wanafunzi kusoma katika mazingira mazuri.

Aidha Katibu Tawala Wilaya ya Kigamboni, Pendo Mahali amesema uhitaji wa madarasa na madawati ni mkubwa mno kutokana na shule hiyo kuwa na wanafunzi 1408 huku uitaji wa madarasa ikiwa 30.

Naibu Kamshina wa walipaKodi wakubwa Eunice Luheluka akizungumza katika hafla hiyo ya kukabidhi madawati Kwa shule ya Msingi Kisarawe II.
Baadhi ya wanafunzi wanaosoma katika shule ya Msingi Kisarawe II wakiwa katika Moja ya madarasa yaliojengwa.