May 3, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

TCU yafungua dirisha la udahili

Na Penina Malundo,TimesMajira ,Online

TUME ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU) , leo imefungua rasmi dirisha la udahili wa Shahada ya kwanza kwa mwaka wa masomo 2020/21.

Udahili huo unatarajia kuanza leo rasmi hadi Septemba 25 mwaka huu.

Katibu Mtendaji wa TCU,Prof.Charles Kihampa amesema dirisha hilo limefunguliwa leo badala ya  Agosti 31,2020, tarehe iliyokuwa imepangwa hapo awali kutokana na matokeo ya kidato ya sita kutoka .

Amesema utaratibu wa maombi ya udahili kwa mwaka wa masomo kwa mwaka 2020/21,utahusu makundi makubwa matatu ya waombaji ikiwemo wenye sifa stahiki za kidato sita,wenye sifa stahiki za Stashahada (Ordinary Diploma) na wenye  sifa stahiki za Foundation Programme ya Chuo Kikuu Huria cha Tanzania.

“Ili kufahamu sifa stahiki kwa  makundi matatu yaliyotajwa hapo juu,waombaji wanaelekezwa kusoma vigezo vilivyooneshwa katika kitabu cha mwongozo cha TCU,”amesema

Wakati huo huo Prof.Kihampa amewataka wananchi kujitokeza kwa wingi katika maonesho ya 15 ya Elimu ya Juu,Sayansi na Teknolojia yanayofanyika katika viwanja vya mnazi mmoja jijini.

Amesema maonesho hayo yanatarajia kufanyika kuanzaia Agosti 31 hadi Septemba 5 mwaka huu ambapo yatapata fursa ya wananchi kuonana ana kwa ana na Vyuo vya elimu ya juu.