May 9, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

TCAA yasherekea siku ya Anga Duniani

Na Penina Malundo, timesmajira

Tanzania imeungana na mataifa mengine katika kusherekea siku za anga duniani huku,Tanzania ikijivunia kuwepo kwa mitambo ya kidigitali ambayo inazidi kufanya anga kuwa salama.

Hayo ameyasema leo jijini Dar es Salaam wakati wa maadhimisho ya siku ya Anga duniani ambapo yameenda sambamba na maandamano yaliyoanza katika Ofisi TCAA na kuishia katika Ofisi hiyo ikiwahusisha wafanyakazi na wanafunzi wa Shule mbalimbali katika kusherekea siku hiyo,Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga (TCAA),Teophory Mbilinyi alisema TCAA inasherekea siku hiyo kwa sababu ya Tanzania ni wanachama w Shirika la Anga Duniani ,lakini pia ilisaini mkataba wa Chicago kupitia mkataba huo shirika la Anga Duniani lilitenga kila Decemba 7 ya kila mwaka iwe ni siku ya kusherekea siku ya Anga Duniani kote.

“Lengo maadhimisho haya ni kukumbushana majukumu yetu kuhakikisha tunasimamia shughuli za usafiri wa anga kikamilifu na kuhakikisha kwamba anga letu na wenzetu wa nchi za jirani yanakuwa salama”amesema na kuongeza.

“Kiujumla Anga letu ni salama kwa sababu tunavifaa na mitambo za kutosha ya kusaidia marubani wa ndege wanavyopita katika anga letu,kwani miaka iliyopita tumefunga rada nne mpya za kuhakikisha anga lote linaonekana na tunamitambo mbalimbali ya mawasiliano ya kati ya marubani na waongoza ndege kuhakikisha anga linakuwa salama wanapokuwa safarini,”amesema.

Amesema wanamafanikio mengi ambapo hivi karibuni kupitia ukaguzi wa usalama Tanzania iliibuka mshindi wa wanne kwa nchi za Afrika katika usalama hivyo ni nchi bora kwa usalama wa anga Anga.

“Kiteknolojia napo tupo vizuri kwa sababu mitambo yote inayotakiwa kuongoza ndege tunayo na rada zilizofungwa ni miongoni mwa rada bora barani afrika tupo vizuri sana mitambo imefungwa nchini nzima ipo salama hata marubani wanaporusha vyombo katika anga la Tanzania wanafurahia kwa sababu wanajua kwamba wapo salama kutokana na mitambo iliyopo nchini,”amesema.

Kwa Upande wake Mkurugenzi Huduma za Uongozaji Ndege ,Flora Mwanshinga amesema alisema kwa eneo lake anajivunia uboreshaji wa mitambo ya kuongoza ndege na wataalamu wa kuongoza ndege.

Amesema katika mitambo hivi karibuni walikuwa na miradi ya kubadilisha mitambo ya sauti kati ya rubani na waongoza ndege ambayo ni mitambo za kidigitali inayowafanya kufanya kazi zao kwa ufasaha.