April 29, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

TBS inavyotekeleza dhamira ya Rais Samia uwezeshaji biashara

Na Jackline Martin,TimesmajiraOnline,Dar

DHAMIRA kubwa ya Serikali ya Awamu ya sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan, ni kukuza uchumi na kuweka mazingira wezeshe ya ufanyaji biashara.

Kutokana na dhamira hiyo ya Serikali, Shirika la Viwango Tanzania limekuwa bega kwa bega na Serikali katika kutekeleza azma ya kuwezesha ufanywaji wa biashara nchini utakaoendana na kuinua viwanda kwa kusimamia ubora wa bidha, kulinda usalama wa mlaji sambamba na kusimamia mapato ya Serikali.

Kwa kutambua hilo,Shirika limeendelea kutekeleza majukumu yake yote kwa kuzingatia weledi na ufanisi wa hali ya juu ili kuhakikisha malengo ya Rais Samia yanafikiwa kwa wakati uliokusudiwa.

Majukumu ya Shirika la Viwango Tanzania yameainishwa katika Kifungu cha 4 (1) (a) – (v) cha Sheria ya Viwango Sura Na. 130. Majukumu (functions) hayo kwa ufupi ni kama yafuatayo;

Kutayarisha na kutangaza Viwango vya ubora vya Tanzania kwenye sekta zote za uchumi. Kipaumbele kimewekwa katika viwango vya kitaifa katika nyanja za nguo, ngozi, kilimo na chakula, madawa (kemikali), uhandisi na mazingira;

Kutekeleza viwango vya ubora vilivyotangazwa kwa kutumia mifumo mbalimbali ya udhibiti ubora kama vile ukaguzi na upimaji wa bidhaa kabla ya kusafirishwa kuja nchini, upimaji wa bidhaa kwa kuzingatia matakwa ya kiwango au ya mzalishaji na usajili wa mifumo ya ubora;

Majukumu mengine ni kuchukua na kupima sampuli za bidhaa zinazokusanywa na wakaguzi wa TBS, kwa lengo la kutekeleza viwango au kwa kuzingatia maombi ya mzalishaji;

Kutoa mafunzo kwa wenye viwanda na biashara juu ya uzalishaji na utoaji huduma bora kwa kuzingatia viwango; na
Kuvifanyia ugezi vipimo vya vifaa vya upimaji viwandani na vya kibiashara katika nyanja za uzito, urefu, ujazo, nishati, halijoto na mengine.

Majukumu hayo yameendelea kutekelezwa kikamilifu chini ya uongozi wa Rais Samia kama ambavyo inaanishwa na Mkurugenzi Mkuu wa TBS, Dkt. Yusuf Ngenya, wakati akizungumza na wahariri wa vyombo vya habari nchini katika mkutano ulioandaliwa na ofisi ya Msajili wa Hazina.

HUDUMA KARIBU NA WANANCHI

Anasema shirika limefanikiwa kusogeza huduma karibu na wananchi kupitia ofisi za kanda saba ambazo ni Kanda ya Kaskazini (Arusha) ,Kanda ya Kusini (Mtwara) ,Kanda ya Nyanda za Juu Kusini (Mbeya).

Nyingine ni Kanda ya Magharibi (Kigoma) ,Kanda ya ziwa (Mwanza) ,Kanda ya Kati (Dodoma) na Kanda ya Mashariki (Dar es Salaam).
Kanda hizi zina ofisi katika mipaka, bandari pamoja na viwanja vya ndege.

UNUNUZI VIFAA VYA MAABARA

Aidha, Dkt. Ngenya amesema Shirika limewekeza kwenye ununuzi wa vifaa vya maabara vya kisasa kwa kutumia fedha za ndani pamoja na misaada kutoka kwa wadau mbalimbali wa maendeleo.

MAABARA ZOTE ZINA ITHIBATI

Kwa upande wa ithibati za umahiri katika maabara, Dkt. Ngenya alisema Shirika lina maabara 12 zilizopo Ubungo Dar es Salaam, ambapo zimehakikiwa na kupatiwa cheti cha ithibati ya umahiri wa kimataifa (accreditation).

“Hatua hiyo inapelekea majibu ya sampuli kutoka katika maabara hizo kuaminika kokote duniani na hivyo kurahisisha biashara,” anasema Dkt. Ngenya.

MFUMO WA KIELEKTRONIKI

Kuhusu utoaji huduma kupitia mifumo ya kielektroniki, alisema
Shirika limetengeneza mifumo ya kielektroniki inayotumika kutoa huduma zake.

“Uanzishwaji wa mifumo ya kielektroniki imewezesha wateja kupata huduma za TBS popote walipo kwa wepesi na haraka hivyo kupunguza gharama kwa wateja,” anafafanua Dkt. Ngenya.

Aidha, amesema imeweka mazingira wezeshi kwa wafanyabiashara na wazalishaji.

VIWANGO VILIVYOANDALIWA

Kwa kipindi cha miaka mitatu, jumla ya viwango 1,721 vya kitaifa viliandaliwa sawa na asilimia 101.2 ya lengo la kuandaa viwango 1,700.

Kwa mujibu wa Dkt. Ngenya viwango hivyo viliandaliwa katika nyanja mbalimbali. Pia anasema TBS imeshiriki katika uandaaji wa viwango vya kibiashara vya Afrika Mashariki na Afrika nzima.

WAJASIRIAMALI WAHUDUMIWA BILA MAIPO

Ameongeza kwamba Serikali kwa kupitia TBS imekuwa ikitenga zaidi ya milioni 250 kwa dhumuni la kuhudumia wajasiriamali wadogo bila ya malipo yoyote.

LESENI ZILIZOTOLEWA

“Kwa kipindi cha miaka mitatu, jumla ya leseni za ubora wa bidhaa 2,106 zilitolewa kwa wazalishaji mbalimbali wa bidhaa hapa nchini sawa na asilimia 105.3 ya lengo la kutoa leseni 2,000. Kati ya leseni hizo, jumla ya leseni 1,051 zilitolewa bure na kwa Wajasiriamali wadogo,”anasema.

Aidha, anasema kwa kipindi cha miaka mitatu, jumla ya wadau 5,789 kutoka mikoa mbalimbali nchini walipewa mafunzo hayo.

“TBS imeendelea kutoa mafunzo kwa wajasiriamali wadogo (MSEs) na wazalishaji ili kuwawezesha kuzalisha bidhaa zinazokidhi matakwa ya viwango vya ubora na usalama na hatimaye kukidhi ushindani wa masoko ya ndani, kikanda na kimataifa,” anasema.

UKAGUZI WA BIDHAA

Anaongeza kwamba Shirika limeandaa utaratibu wa kukagua viwanda vyote hapa nchini ili kuhakikisha kwamba vinazalisha bidhaa zenye ubora unaotakiwa.

Alifafanua kwamba kwa kipindi cha miaka mitatu, jumla ya leseni za ubora wa bidhaa 2,106 zilitolewa kwa wazalishaji mbalimbali wa bidhaa hapa nchini sawa na asilimia 105.3 ya lengo la kutoa leseni 2,000.

Kuhusu ukaguzi wa bidhaa zinazotoka nje ya nchi, Dkt. Ngenya, anasema TBS hudhibiti ubora wa bidhaa zinazoingizwa nchini kutoka nje kwa kutumia mfumo wa Pre-Shipment Verification of Conformity to Standards (PVoC) pamoja na kufanya ukaguzi pindi bidhaa zinapowasili nchini (Destination Inspection).

Kwa kipindi cha miaka mitatu, jumla ya shehena 100,851 kabla hazijaingizwa nchini sawa na asilimia 99 ya lengo la kukagua shehena 102,083. Pia, jumla ya bidhaa 151,570 kutoka nje ya nchi zilikaguliwa baada ya kufika nchini sawa na asilimia 77 ya lengo la kukagua bidhaa 197,417.

Anasema TBS hudhibiti ubora wa bidhaa zinazoingizwa nchini kutoka nje kwa kutumia mfumo wa Pre-Shipment Verification of Conformity to Standards (PVoC) pamoja na kufanya ukaguzi pindi bidhaa zinapowasili nchini (Destination Inspection).

Anasema kwa kipindi cha miaka mitatu, jumla ya shehena 100,851 zimekaguliwa kabla hazijaingizwa nchini sawa na asilimia 99 ya lengo la kukagua shehena 102,083.

BIDHAA ZILIZOKAGULIWA

Pia, anasema jumla ya bidhaa 151,570 kutoka nje ya nchi zilikaguliwa baada ya kufika nchini sawa na asilimia 77 ya lengo la kukagua bidhaa 197,417.

Aidha, anasema limekuwa likifanya kaguzi mbalimbali za kushtukiza katika masoko ya ndani TBS hufanya kaguzi za mara kwa mara sokoni na viwandani kwa ajili ya kuhakikisha bidhaa zilizopo zinakidhi matakwa ya viwango husika.

Anasema TBS pia hushirikiana na taasisi nyingine za Serikali kama TRA, FCC, Ofisi ya Rais TAMISEMI, Jeshi la Polisi pamoja na vyombo vingine vya usalama kufanya ukaguzi ili kubaini bidhaa zisizokidhi matakwa ya viwango na kuchukua hatua stahiki.

KUTOA ELIMU

Dkt. Ngenya anasema TBS hutoa elimu kwa umma kupitia njia mbalimbali ili kukuza uelewa juu ya masuala ya viwango na udhibiti ubora. Njia hizo ni pamoja na: Kushiriki katika makongamano, maonesho, warsha na semina; Kuandaa mikutano na wadau wa masuala ya viwango (Stakeholder’s meeting); Kuendesha kampeni za elimu kwa umma katika ngazi za wilaya na mashuleni;

Kutoa elimu kutumia vyombo vya habari na mitandao ya kijamii;
Kuandaa matangazo, majarida na vipeperushi; na Kutoa mafunzo mbalimbali kuhusu masuala ya ubora na usalama.

Anaongeza kwamba TBS hutoa elimu kwa umma kupitia njia mbalimbali ili kukuza uelewa juu ya masuala ya viwango na udhibiti ubora. Njia hizo ni pamoja na:

Kushiriki katika makongamano, maonesho, warsha na semina;
Kuandaa mikutano na wadau wa masuala ya viwango (Stakeholder’s meeting); Kuendesha kampeni za elimu kwa umma katika ngazi za wilaya na mashuleni; Kutoa elimu kutumia vyombo vya habari na mitandao ya kijamii; Kuandaa matangazo, majarida na vipeperushi; na Kutoa mafunzo mbalimbali kuhusu masuala ya ubora na usalama.

UJENZI WA MAABARA ZA KANDA

Aidha, Shirika linatarajia kuanza ujenzi wa maabara ya kisasa katika kanda ya Ziwa (Mwanza) na kanda ya kaskazini (Arusha). Maabara ya kanda ya ziwa inatarajiwa kuhudumia mikoa sita ambayo ni Mwanza, Kagera, Mara, Geita, Shinyanga na Simiyu. Aidha, maabara ya kanda ya Kaskazini inatarajiwa kuhudumia mikoa minne ambayo ni Arusha, Kilimanjaro, Tanga na Manyara.

Shirika linatekeleza mradi wa ujenzi wa Makao Makuu ya Shirika na maabara (Viwango House – Dodoma). Maabara hii itahudumia mikoa mitatu ya kanda ya Kati ambayo ni Dodoma, Singida na Tabora pamoja na mikoa mingine ya karibu.