April 25, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Tanzania zapangiwa Botswana, Namibia

Na Mwandishi Wetu, TimesMajira Online

TIMU ya Taifa ya Tanzania ya wasichana wenye umri wa miaka 17 imepangwa kuanza na Botswana katika mchezo wa raundi ya kwanza wa kusaka tiketi ya kucheza Fainali za Kombe la Dunia kwa wasichana wenye umri huyo (U-17 FIFA Women’s World Cup Qualifier 2022 India) katika mchezo utakaochezwa  kati ya Januari 13-29.

Pia timu ya Taifa kwa wachezaji wenye umri chini ya miaka 20 wenyewe watatupa karata yao dhidi na mshindi wa mechi kati ya Djibouti na Eritrea katika mzunguko wa pili wa kufuzu Kombe la Dunia ‘African Qualifiers FIFA U 20 Womens World Cup Costa Rica 2022’ huku timu ya Taifa ya wakubwa ‘Twiga Stars’ wenyewe wakipangwa kucheza na Namibia katika mzunguko wa kwanza wa kuwania kufuzu kucheza Kombe la Mataifa Afrika kwa wanawake ‘Women Africa Cup of Nation (AFCON)’.

Katika dhoo iliyochezeshwa jana mchana Cairo, Misri, timu nne kutoka Baraza la Vyama vya Soka Afrika Mashariki na Kati (CECAFA) zimepangwa katika raundi ya kwanza ambapo mbali na Tanzania, Rwanda wamepangwa watakutana na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Eritrea itawakabili Sudan Kusini huku timu ya Taifa ya Kenya itachuana na Guinea ya Ikweta. kati ya timu kumi utachezwa kati ya Januari 13-29.

Akichezesha dhoo hiyo akisaidiwa na Nadine Ghazy, Mkurugenzi wa mashindano wa Shirikisho la Soka Barani Afrika (CAF), Khaled Nassar amesema, droo hiyo imehusisha timu 29.

Timu zitakazoshinda raundi ya kwanza zitaingia raundi ya pili ambayo Djibouti itakutana na Burundi, Tanzania itacheza dhidi ya Botswana, Uganda itavaana na Ethiopia, mshindi kati ya Eritrea na Sudan Kusini atakutana na Cameroon wakati mshindi wa mchezo kati ya Kenya dhidi ya Guinea ya Ikweta atakutana na Afrika Kusini.

Mshindi kati ya DR Congo na Rwanda atapambana na Nigeria katika raundi ya pili na kulingana na CAF raundi nne zitachezwa kubaini ni timu gani tatu zinazostahiki kuwakilisha Afrika.

Itakumbukwa kuwa awali michuano hiyo ya Kombe la Dunia la Wanawake la U-17 la FIFA India ilipangwa kufanyika kati ya Novemba 2020 lakini yalilazimika kuahirishwa kutokana na mlipuko wa Covid 19