June 2, 2026

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Mtatifikolo (CCM) aibuka kidedea jimbo la Isimani

Na Mwandishi wetu,Iringa

‎Mgombea wa ubunge wa Jimbo la Ismani kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Emmanuela Mtatifikolo ameibuka mshindi baada ya kupata kura 70,905 kati ya kura halali 75,874 zilizopigwa katika uchaguzi wa jimbo hilo.

‎Matokeo hayo yametangazwa rasmi leo Juni 2, 2026 na Msimamizi wa Uchaguzi wa Jimbo la Ismani, Caroline Ang’wen Otieno, baada ya kukamilika kuhesabu na kujumlisha kura kutoka vituo mbalimbali vya kupigia kura ndani ya jimbo hilo.

‎Kwa mujibu wa matokeo yaliyotangazwa, jumla ya wapigakura waliojiandikisha katika Jimbo la Ismani walikuwa 89,753, huku wapigakura 76,556 sawa na asilimia 85.3 wakijitokeza kushiriki uchaguzi. Kati ya kura hizo, kura halali zilikuwa 75,874 na kura 684 zilikataliwa.

‎Matokeo yanaonesha kuwa Emmanuela Mtatifikolo wa CCM alipata kura 70,905, sawa na asilimia 93.5 ya kura zote halali zilizopigwa, na hivyo kuibuka mshindi kwa tofauti kubwa dhidi ya wagombea wa vyama vingine.

‎Matokeo ya wagombea wengine yalikuwa kama ifuatavyo: AAFP kura 186, ADA TADEA kura 189, ADC kura 775, CHAUMA kura 1,512, CUF kura 802, DP kura 139, MAKINI kura 137, NCCR Mageuzi kura 155, NLD kura 147, NRA kura 136, SAU kura 69, TLP kura 73, UDP kura 82, UND kura 28, UPDP kura 43 na CCK kura 162.


‎Uchaguzi mdogo wa Jimbo la Isimani umefanyika kutokana na kifo cha aliyekuwa Mbunge wa jimbo hilo, William Lukuvi, kilichotokea Machi 25, 2026.