
Na Israel Mwaisaka, Rukwa.
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa, Charles Makongoro Nyerere, ameridhishwa na maendeleo ya ujenzi wa shule mpya ya Msingi Milundikwa ya Mkondo Mmoja katika Halmashauri ya Wilaya ya Nkasi, unaolenga kuimarisha maandalizi ya utekelezaji wa Sera ya Elimu na Mafunzo ya Mwaka 2014 Toleo la 2023.
Akikagua mradi huo Jana June 1, 2026, Makongoro alisema Serikali inaendelea kuboresha miundombinu ya elimu ili kuweka mazingira wezeshi ya utekelezaji wa sera hiyo kuanzia mwaka wa masomo 2028.
Alisema mwaka 2028 wahitimu wa elimu ya msingi ya miaka sita pamoja na kundi la mwisho la wahitimu wa elimu ya msingi ya miaka saba wataanza kidato cha kwanza kwa pamoja, hivyo kuhitajika maandalizi ya mapema ya miundombinu ya elimu.
Alidai kuwa kwa Sasa wao kama Serikali ni kutaka kuona maandalizi ya kutosha yanafanyika ili kuweza kumudu kuwapokea wahitimu wa darasa la Saba na wale la sita katika kuanza Kidato Cha kwanza kwa pamoja na ndiyo maana wanahakikisha kuona miundo mbinu ya shule za sekondari inaimarishwa ili kukabiliana na mazingira hayo.
Na alifafanua kuwa michakato ya utekelezwaji wa miradi mbalimbali ya kisekta wilayani Nkasi imekua na tija kubwa kutokana na utekelezwaji wa miradi hiyo kwa ubora unaoridhishwa na kuwa hilo linatokana na mshikamano uliopo wa viongozi kuanzia ngazi ya chini na kutaka mshikamano huo uendelee ili tuweze kupata miradi yenye tija.
Katika ziara hiyo, Mkuu wa Mkoa pia amekagua maendeleo ya ujenzi wa Kituo cha Afya Chala, ukamilishaji wa mabweni mawili katika Shule ya Sekondari Chala, Mradi wa Maji wa Namanyere pamoja na ujenzi wa Shule ya Amali ya Mkoa.

More Stories
Mtatifikolo (CCM) aibuka kidedea jimbo la Isimani
NMB yatumia Twenzetu kwa Yesu kuendeleza elimu ya Fedha
Songwe waimarisha mifumo ya ufuatiliaji tishio la Ebola