Na Mwandishi wetu,Timesmajira
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade), Ephraim Balozi Mafuru, leo amekutana na Balozi wa Serbia nchini Tanzania, Jovica Topalović, katika ofisi za TanTrade jijini Dar es Salaam, kwa lengo la kuimarisha ushirikiano wa kibiashara na uwekezaji kati ya Tanzania na Serbia.
Akizungumza baada ya kikao hicho, Mafuru amesema TanTrade inaendelea kutekeleza jukumu lake la kufungua masoko na kuunganisha wafanyabiashara wa Tanzania na wenzao wa kimataifa.
Ameeleza kuwa ushirikiano huo utalenga kuwawezesha wakulima, wazalishaji na wafanyabiashara wa Tanzania kupata fursa za biashara katika soko la Serbia, sambamba na kukuza ushirikiano katika sekta ya viwanda ili kuongeza thamani ya bidhaa na kuchochea maendeleo ya uchumi wa nchi.

Kwa upande wake, Balozi wa Serbia nchini Tanzania, Jovica Topalović, ameishukuru TanTrade kwa mapokezi mazuri na kueleza kuwa Serbia ipo tayari kuimarisha ushirikiano wa kiuchumi na Tanzania.
Amesema ushirikiano huo utafungua fursa mpya za biashara, uzalishaji,Kilimo, teknolojia ya viwanda pamoja na uhifadhi mazao ( Cold room facilities) hususan kwa mazao ya Nyama, Samaki na Matunda.


More Stories
Wakulima waliowezeshwa na TADB waeleza mafanikio yao nanenane
Serikali kuendelea kuunga mkono Taasisi zinazowezesha kilimo
Ukaguzi wa migodi waimarisha Usalama,Uhifadhi wa Mazingira