Na Mwandishi Wetu,Timesmajira
TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa ( TAKUKURU) Mkoa wa Kinondoni imesema imeweza kuokoa zaidi ya mapato ya sh.milioni 500 zilizopotea kwa miezi mitatu kutokana na ushuru wa huduma.
Akitoa taarifa ya mafanikio ya utendaji kazi wa Taasisi hiyo kwa waandishi wa habari leo Naibu Mkuu wa TAKUKURU Kinondoni Elizabeth Mokiwa amesema kwa kipindi cha kuanzia Januari hadi Machi 2026 wameweza kudhibiti upotevu wa mapato ya sh.563,663,820.15 ya ushuru wa huduma.
“Kwa kushirikiana na Mkurugenzi wa Manispaa ya Kinondoni TAKUKURU tumeweza kufanikiwa kudhibiti upotevu wa kiasi hicho cha fedha ambazo baadhi ya wafanyabiashara wasio waaminifu walikwepa kulipa,” amesema
MokiwaAmesema udhibiti huu umefanyika baada ya kupokea taarifa za kuwepo kwa baadhi ya wafanyabiashara wasiolipa ushuru wa huduma kulingana na mauzo yao ya mwaka
” Kukwepa kulipa ushuru huu husababisha upotevu wa mapato yanayostahili kukusanywa na halmashauri na kusababisha kutokufikiwa kwa malengo ya makusanyo yaliyotarajiwa,”amesema
Amesena baada ya TAKUKURU Kinondoni kufanya ufuatiliaji na kuwataka wafanyabiashara kulipa ushuru wa huduma wanayodaiwa kupitia control namba ya halmashauri hiyo wafanyabiashara walianza kulipa fedha hizo.
Amezungumzia ufuatiliaji wa matumizi ya fedha za utekelezaji wa miradi ya maendeleo kwa kusema kuwa TAKUKURU Kinondoni ilifanya kikao kazi na watekelezaji wa miradi wakiwepo wakandarasi ili kuhakikisha miradi inakamilika ndani ya muda
“Katika kutekeleza jukumu hili TAKUKURU Kinondoni tulifanya kikao kazi na watekelezaji wa miradi wakiwemo wakandarasi,washauri na wasimamizi wa miradi ili kuhakikisha miradi inakamilika ndani ya muda wa nyongeza waliopatiwa kwa kuzingatia ubora, matakwa na usalama kama ilivyoelekezwa na TAMISEMI,” amesema Mokiwa
Amesema kwa kipindi cha Januari hadi Machi 2026 wamefuatilia matumizi ya fedha za utekelezaji wa miradi ya maendeleo saba ambapo mitatu ikiwa katika sekta ya afya ambayo ni ujenzi wa ghorofa moja yenye wodi ya wazazi na sehemu ya upasuaji katika Zahanati ya Ndumbwi
Ingine ni jengo la magonjwa ya kuambukiza katika Hospitali ya Wilaya ya Kinondoni iliyopo Mabweoande na ujenzi wa ukuta katika hospitali hiyo yenye jumla ya sh 1,625,960,706″ Vilevile miradi minne yenye thamani ya sh. 340,400,000 katika sekta ya elimu ambayo ni ujenzi wa madarasa na matundu ya vyoo katika shule ya sekondari Makabe, shule ya msingi Luguruni na ujenzi wa jengo la ofisi katika Shule ya Sekondari Makabe.
Aidha ameongeza kuwa kupitia elimu waliyotoa kwa umma wananchi na wadau imesaidia kuongeza ufanisi wa usimamizi wa miradi ya maendeleo wananchi pia wamehamasika kutoa taarifa za vitendo vya rushwa katika ngazi ya mitaa na kata.
Amezungumzia uchunguzi wa mashitaka kwa kusema kuwa malalamiko 78 yalipokelewa katika kipindi hicho ambapo 26 yalihusu rushwa na kwamba uchunguzi wake unaendekea uko katika hatua mbalimbali.
Anaitaja mikakati ya TAKUKURU Kinondoni kuwa ni pamoja na kuendelea kufuatilia matumizi ya fefha za miradi ya maendeleo, kuendelea kutoa elimu kwa wananchi na wadau na kuendelea kufuatilia utekelezaji wa mapendekezo ya program ya takukuru rafikiHata hivyo amewataka wananchi wote kujiepusha na vitendo vya rushwa na kushiriki kikamilifu katika kuzuia vitendo hivyo kwenye maeneo yao.

More Stories
Serikali yafikisha Umeme Katika Migodi 289 ya Wachimbaji Wadogo
Vipaumbele tisa bajeti Maliasili na Utalii
Kichwa cha Marehemu James Temba Mwanafunzi wa IFM chapatikana